Marekani inaweza kuivamia Iran kwa silaha za nyuklia ndani ya siku chache

Kama habari ilivyoandikwa itakuwa Baada ya siku Saba kuanzia leo basi dunia itaingia kwenye matatizo makubwa sana
Hasara ya vita vya Nuclear ni mkubwa zaidi, bora maelewano
Kama US ataamua hivyo basi Kila nchi yenye Nuclear itaamua nayo kutumia
 
Umeandika hivi ili kujihami au unataka kuficha nini? Au unataka kumuonyesha Nani kuwa na wewe unajua kiingereza? Au unataka na sisi tujue wewe unajua ku Copy & Paste?
 
Asilimia 99 haiwezi kutokea. China, Russia na N. Korea hazina unyonge

US anachofanya sasa ni kutafuta mshirika mwenye nguvu kama China na Russia, akikosea akaipiga Iran na nyuklia ndo itakua mwisho wa US kama taifa lenye nguvu .
Wamatumbi tunajua uwezo wa kijeshi wa mataifa yote duniani.
 
ambako idara za kijasusi za Israel zinadai kuwa serikali ya Iran imeanzisha tena mpango wake wa urutubishaji wa madini ya urani kwa ajili ya shughuli za nyuklia.
Imeanzisha? Si Israel walisema nuclear program ya Iran imesharudishwa miaka 20 nyuma? Na Trump alisema satellite zinaangalia masaa 24 kwamba mtu yeyote akisogelea mitambo iliyolipuliwa ili kuhamisha enriched uranium atamalizwa, sasa pickaxe imewezekanaje??

Hao Israel wanatafuta tu sababu ya kuingia vitani ili Netanyahu abaki madarakani
 
Watu wanaiona Iran kama Taifa flani hivi superior saana hata US atumie Nuclear. Ni mawazo mfu hayo, US na Israel wataitandika Iran silaha za kawaida tu.
Sasa mbona regime change imewashinda mpaka leo?

Si mlituambia nuclear capabilities za Iran zimemalizwa, sasa hii pickaxe inafanyaje kazi?
 
Wachina na mambo yao ya kichina.
Maneno mengi vitendo 0.
Ingekua kauli kutoka Moscow, Pyongyang au Tehran ningeamini
Vitendo 0? Hivi si ndio hawa walimsaidia Vietnam na Korea kumtandika USA, so hawatanii
 
Asilimia 99 haiwezi kutokea. China, Russia na N. Korea hazina unyonge

US anachofanya sasa ni kutafuta mshirika mwenye nguvu kama China na Russia, akikosea akaipiga Iran na nyuklia ndo itakua mwisho wa US kama taifa lenye nguvu .
Hayo ni mafundisho yako binafsi, amekufa ayatollah hakuna chochote kilichotokea. Anaweza akapigwa nyuklia na hakuna wa kufanya chochote
 
Kosa langu lipi? Kuleta taarifa au kupost usichopenda?
Acha papara yatulize hayo Majini yako!! Hakuna sehemu yoyote paliposema Marekani itatumia silaha za Nuclear kuishambulia Iran sana sana ni wewe kuongeza chumvi ili mboga ikolee munyu lakini ukweli hizo ni Propaganda Uchwara kabisa hazina kichwa wala miguu!!
 
Kama inauma chomoa
 
du ngoja nipite kimya
Asilimia 99 haiwezi kutokea. China, Russia na N. Korea hazina unyonge

US anachofanya sasa ni kutafuta mshirika mwenye nguvu kama China na Russia, akikosea akaipiga Iran na nyuklia ndo itakua mwisho wa US kama taifa lenye nguvu .

Iran sio wajinga
Wakipiga hiyo nyuklia vita vyake vitakavyo tokea madhara yake sio kidogo
 
Kwa hiyo wamefeli mpaka wameamua kutumia "ile kubwa"?. Kumbe yale mavyumavyuma, sijui ma F-35. sijui ma mameli ya kivita hamna kitu
 
US wamekuwa maneno mengi kama mashangingi wa Magomeni.Mbona Venezuela walifanya jambo chapu tuu.
 
Nilimsikia Trump akizungumzia kutumia kombora la MOAB.. Massive Ordinance Air Blast wengine huita A.KA yake kama Mother Of All Bombs... GBU 43/B...



Uhalisia ni kwamba US na Israel walichofanikisha hadi sasa ni kufungwa kwa mlango bahari wa Hormuz...

Netanyahu bado anatafuta namna yeyote abaki kwenye kiti, na moja ya njia yake kubaki kitini ni kuanzisha hayo mashambulizi na Iran...

Hivi Netanyahu kwanini anaogopa sana kutoka kitini? Kuna kipi kimejificha? Mbona anahangaika sana?

Inashangaza sana...

Uzuri Iran imesema itajibu..

Trump anafuata maelekezo ya Netanyahu ili wasije kuachia faili zake za Epstein...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…