Marekani inaweza kuivamia Iran kwa silaha za nyuklia ndani ya siku chache

USA hana bomu ya kulipua pale zaidi ya nyuklia ,so wanapiga hesabu kwa sababu wanawza kupiga wakaambulia hola ,huku jamaa akalipiza .
Iyo nyuklia haitosaidia hata tone kufikia kile kinu

Tujiandae tu na vita ya tatu ya dunia
 
Kwa mtazamo wangu israel inaenda kufutika pale mashariki ya kati baada ya ilo tukio la nyuklia
 
Hayo ni mafundisho yako binafsi, amekufa ayatollah hakuna chochote kilichotokea. Anaweza akapigwa nyuklia na hakuna wa kufanya chochote
Unaijua nyuklia? au unafikiri yale waliyokua wanarushiana ndo mabomu ya nyuklia
 
Asilimia 99 haiwezi kutokea. China, Russia na N. Korea hazina unyonge

US anachofanya sasa ni kutafuta mshirika mwenye nguvu kama China na Russia, akikosea akaipiga Iran na nyuklia ndo itakua mwisho wa US kama taifa lenye nguvu .
Hivi mzee unaichukuliaje US?
 
Mkuu, US ana option moja mbali na hiyo nuclear. Uwezekano wa kupiga kutumia nuclear bado ni mdogo japo inaweza ikawa ni option pia.

1. Akitumia nuclear ana advantage kwamba 100% pickaxe imeangamia na hilo eneo halitaweza tena kutumika kurutubisha Nuclear. B61-12 inapodondoka inasababisha joto kali saaana ktk huo mlima, hii itapelekea kila kilichohifadhiwa humo ndani kuharibika, pia ule mpasuko wake utafanya vyumba kadhaa vilivyo chini ya mlima huo kuharibika.

2. GBU 57 bado ni option inayowezekana kutumika kutimiza lengo lao, na hii ndio option kwa 99% watatembea nayo. Pickaxe inaweza ikadondoshewa GBU 57 zaidi ya 20 au 30. Hii itafanya kusimamisha mradi huo kwa zaidi ya miezi 3 hadi 6. Kadri watakavyodondosha kwa ufasaha mabomu hayo na kwa wingi ndivyo watakavyoharibu zaidi. Nimeona wanasema kuna uwezekano bomu la 1 litakapotua, la 2, la 3 na kuendelea litadondokea hapo hapo hadi kufikia lengo hilo. Pia pamoja na kupiga milango ya kuingilia pickaxe na zile ventilazation chambers.

Sisi yetu macho, ngoja tuone kipi kitatokea.
 
kwann hawa Iranian wasiingize jeshi Israel moja kwa moja wanakera kila cku kusubiria kuchokozwa ...
 
Hayo ni mafundisho yako binafsi, amekufa ayatollah hakuna chochote kilichotokea. Anaweza akapigwa nyuklia na hakuna wa kufanya chochote
Ile miji ya Israel na uwekezaji wa Marekani aliulipua nani!? Au alilipua shemeji yako?
 
Hii option USA hawezi kuitumia kamwe wacha delusions. Iran ni karata muhimu sana ya maslahi ya Urusi na China pale mashariki ya kati. Unadhani hao super power wawili watamuacha tu US atumie nuclear?
Hizo GBU-57 zishatumika Natanz,Fordow na hazijafanya lolote mengine hadi Iran ameyachukua ambayo hayajaweza kulipuka.
 
Hakuna taifa lenye haki ya kutumia nguvu za kijeshi kulazimisha matakwa yake kwa jingine. Iran ina haki ya kulinda mamlaka yake suluhisho ni diplomasia, si vitisho vya nyuklia.
Wapi bhana wewe rais wao kauwawa vibaya na haohao USA hao china walifanya nini..rais wa venezuela ametekwa kweupe ikulu nani aliongea..dunia inawenyewe kama Tanzania ilivyo na wenyewe
 
Wanyukane tu hakuna namna...
 
China haikuwahi kwenda kinyume na maneno yake. Pia unatakiwa ufahamu hata vita hii China iliisaidia Iran kwa namna moja ama nyingine.
China washaongea sana unakumbuka mwaka juzi walisema spika wabunge la marekan akikanyaga Taiwan watamlipua chaajabu bidada alishuka Taiwan nachina ikaishia kulalama tu
 
Changamoto pia ni air defence za muIran hivyo watafanya kwa haraka haraka pia haina uhakika sana Kawa hizo nyuklia hazihamishwi kama mtu anataka kukuibia kuku wako na una option iweje uweke kuku zako zote pamoja? Iran sio mjinga
 
Iyo nyuklia haitosaidia hata tone kufikia kile kinu

Tujiandae tu na vita ya tatu ya dunia
Hiyo nuclear inayozungumziwa hapo ni tactical nuclear, ni ndogo ila ikipigwa ktk mlima wa pickaxe, mlima wote utashikwa na joto kali sana saaana, hatimae kila kilicho ndani ya mlima kitaungua kwa joto lile, tabaka la jiwe la mlima litashikwa na joto kiasi kwamba hata zile chambers za ndani zitamomonyoka kwa kiasi kingi cha joto.

Pili, mifumo ya hewa na umeme itakufa on spot kutokana na joto na mshindo mkubwa wa kwenda chini wa nuclear, b61-12 ikipigwa, madhahara yake yanashuka chini ya ardhi zaidi na sio kuenea kwa juu kama zilivyo nuclear zingine.

Pia Uranium zote ambazo zimehifadhiwa humo ndani nazo pia zitaharibika.

Nuclear ikipigwa hapo maana yake hilo eneo hakuna binadamu atakayeweza kusogelea eneo hilo kwa zaidi ya mwaka mzima.

B61-12 ndio bomu litakalowapa 100% guarantee US ya ufanisi wa mission yao.

USICHUKULIE BOMU LA NUCLEAR kama bomu la kawaida, ndio maana Israel inahaha Iran asimiliki hizo silaha, weka ushabiki pembeni, Nuclear ni kitu kingine kabisa kabisa.
 
Wapi bhana wewe rais wao kauwawa vibaya na haohao USA hao china walifanya nini..rais wa venezuela ametekwa kweupe ikulu nani aliongea..dunia inawenyewe kama Tanzania ilivyo na wenyewe
Madulo kachukuliwa akiwa anatumia vifaa vya ulinzi kutoka China na Russia.

China anahangaika kila siku kwa Taiwan na anajua fika US ndie anayemfadhili Taiwan.

Russia vita vimefika nchini kwake akijua kabisa US ndiye anayempa silaha Ukraine. Mwanzo mwa vita Putin alitangaza ole wake atakayemsaidia Ukraine, atammaliza. Nchi za ulaya zikiongozwa na US zimepeleka sana silaha Ukraine na hakuna kitu Putin alifanya.
 
China washaongea sana unakumbuka mwaka juzi walisema spika wabunge la marekan akikanyaga Taiwan watamlipua chaajabu bidada alishuka Taiwan nachina ikaishia kulalama tu
Nakumbuka hii mkuu, China alitoa mkwara mkali saana.
 
Umeandika hivi ili kujihami au unataka kuficha nini? Au unataka kumuonyesha Nani kuwa na wewe unajua kiingereza? Au unataka na sisi tujue wewe unajua ku Copy & Paste?
Weye mlokole mvaa kitenge mjinga kama hujui au huelewi lugha ni tatizo lako
Toka hapo kigangoni Manzese ukamuokoe basha wako kashindwa uchaguzi anatapa tapa kutaka kuangamiza hao walokole wenzio


Hili ni bomu lenye nguvu sawa na mara 27 ya bomu lililopigwa Hiroshima!!!!
Kituo cha nyuklia kilichopo katika Mlima Pickaxe pamoja na uranium iliyorutubishwa viko kwenye kina cha ndani ya mlima kisichopungua mita 100, na kwa mujibu wa baadhi ya makadirio, kina hicho kinazidi hata mita 300.

Bomu la nyuklia halitaweza kupenya kina cha zaidi ya mita 6 kwa makadirio ya juu kabisa. Ndiyo, litasababisha mwangwi mkubwa ndani ya miamba na muundo wa kijiolojia wa mlima huo, lakini uwezekano wa kufanikiwa kuharibu shabaha hauzidi asilimia 20, hata kwa makadirio ya juu kabisa!

Kwa upande mwingine, bomu lisilo la nyuklia la GBU-57 lina uwezo wa kupenya hadi mita 60 ndani ya miamba. Lakini kwa mlima kama Pickaxe na kina ambacho kituo hicho kipo ndani yake, bado itakuwa vigumu mno kuharibu shabaha hiyo.

Maana yake ni kwamba, hata kama Trump atapagawa kabisa na kuamua kurusha bomu la nyuklia lenye nguvu kubwa kama B61-11, au kudondosha bomu kubwa kuliko yote, GBU-43/B, hilo litakuwa ni shambulio la maonyesho tu na kujionesha kwa nguvu, bila kupata matokeo yoyote halisi ardhini.

Kwa hiyo, matokeo yatakuwa yapi?
Iran itateketeza kila kitu chenye uoto wa kijani na hata kilichokauka katika eneo lote la Ghuba, na huenda ikapakia uranium iliyorutubishwa kwa kiwango cha asilimia 60 kwenye makombora machafu (dirty missiles) na kuyatumia kushambulia nchi za Ghuba au hata Israel.

+ Putin atapata ujasiri na kucheza kwa furaha huko Moscow kwa sababu atakuwa amepata uhalali wa kumaliza vita vya Ukraine kwa mashambulizi ya nyuklia. Yaani, Trump ametumia silaha hizo dhidi ya Iran, kwa hiyo sasa kila mmoja wetu anaweza kuzitumia.

+ Xi Jianping atapata ujasiri na kwa furaha huko Beijing. Kwa sababu mantiki ni ileile: ikiwa Taiwan itamletea shida, atarusha bomu la nyuklia moja kwa moja kwenye koo lake na kuizika ardhini.

+ Na kila kona ya dunia, rafiki yetu Kim Jong-un, kiongozi wa Korea Kaskazini, atatoka kwa furaha, kwa sababu naye atakuwa amepata uhalali wa kuishambulia Korea Kusini na mtu yeyote duniani asiyependa sura yake.

+ Hatari ya mionzi ya nyuklia itasambaa hadi katika nchi jirani, na kusababisha janga ambalo halijawahi kushuhudiwa katika historia.
 
Huu ulioandika ni UHARO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…