JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Katika mahojiano maalumu na BBC Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright alieleza namna ambavyo Marekani inavyoguswa na tishio la usalama katika baadhi ya mipaka ya Tanzania ikiwemo eneo la mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
Aidha ameelezea athari ya mabadiliko ya tabia nchi lakini pia hatua iliyopigwa na serikali ya Tanzania katika kukuza demokrasia.
Balozi Wright alisema, “Kimsingi Marekani inaguswa na masuala ya kiusalama ya dunia nzima, na hata ukiangalia masuala ya kiusalama katika mipaka ya kusini mwa Tanzania. Kama Balozi natambua na kuweka suala hilo kuwa kipaumbele cha ubalozi wangu…
…tunafikiri kwamba masuala haya yasipoangaliwa kwa umakini yanaweza kuleta madhara, hivyo tumekuwa tukijielekeza katika masuala haya, na tunafurahi kuona Rais Samia Suluhu ameushirikisha umoja wa nchi za kusini mwa SADC ili ziweze kutoa suluhisho na sisi tupo tayari kutoa ushirikiano wetu wa kimawazo pale utakapo hitajika.”
Hali ya Demokrasia Tanzania
Balozi amepongeza jitihada za serikali ya Tanzania ya sasa kutokana na mazungumzo ambayo yamekuwa yakiendelea kati ya serikali, chama tawala na vyama wa upinzani.
Balozi huyo alisema,Rais Samia ameonyesha jitihada kubwa katika suala zima la maridhiano ya kisiasa amekuwa na mikutano kadha kukutama na viongozi wa upinzani ili kupata mariadhiano ya kisiasa na kupata maoni yao hivyo sisi Marekani tunasimama na serikali na kwamba tunaunga mkono kufikiwa kwa maridhiano hayo.
Athari za mabadiliko ya tabia nchi
Hata hivyo Balozi Donald amezungumzia nia ya Marekani kuisadia Tanzania katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema, “Naomba niseme kwamba suala la mabadiliko ya tabia nchi ni janga linazoathiri mataifa mbali mbali duniani, hivyo mabadiliko ya tabia nchi ni eneo muhimu ambalo tunaliangazia pia,na ambalo limekuwa likisababisha ukame,katika ukanda wote wa nchi za jangwa la Sahara,ilikuwa ni mwaka mmoja tu uliopita Kenya ilikumbwa na janga nzige waliodhoofisha uzalishaji katika mashamba ya mawese…
“…kwa hiyo kutaendelea kuwepo na majanga kama hayo hivyo tunataka kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha tunatoa msaada,” alisema Balozi huyo.
Chanzo: BBC