Marekani kasimamisha michango mashirika ya afya kwanini nchi nyingi zinalaumu, kwanini nchi nyingi zinazonufaika na misaada zinakwepa michango ?

wastani kwa idadi

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2024
Posts
503
Reaction score
1,432
Marekani inachangia kila mwaka dola milioni 500 (shilingi Trilioni 1.2) kwenye shirika la afya duniani.

mataifa mengine yana watu wengi zaidi mfano China, ina watu zaidi ya bilioni 1 inachangia Dola milioni 20 (shilingi bilioni 50) .

Marekani baada ya kuona pesa zao zinafujwa, Trump kaamua kusitisha michango.

Kelele na Lawama nyingi zimezuka baada ya Marekani kusitiha misaada kukiwa na malalamiko ya ufinyu wa bajeti.

Nchi za Afrika zimekuwa mstari wa Mbele kutoa Lawama lakini ni viongozi hao wanaolalamika wanaongoza kwa kutapanya misaada inayotolewa kila mwaka inayoishia mifukoni mwa wachache.

Sio shirika la afya tu, Kwenye ulinzi wa nchi za Ulaya (NATO) Marekani ndie anaechangia zaidi, nchi zote za ulaya zinategea kukwepa michango.
 
Sio shirika la afya tu, Kwenye ulinzi wa nchi za Ulaya (NATO) Marekani ndie anaechangia zaidi, nchi zote za ulaya zinategea hazichangii fair share.
Trump kusaini Agizo linalokataza Waliobadili Jinsia kutumikia Jeshi ☞ Trump kusaini Agizo linalokataza Waliobadili Jinsia kutumikia Jeshi - Fntaz
 
Marekani inaongoza kuiba rasilimali duniani kote,huo siyo msaada bali kidogo katika faida kubwa aibayo
Jihadists mkiambiwa mthibitishe wanavyoiba mnakuwa mabubu, nyie ndio wale wale kijijini akitokea mtu moja tajiri mnasema ni mwizi mara sijui freemason.

Watu wa hovyo sana nyie, hamtaki kupigana muondokane na hali duni mliyonayo ni kukaa tu na kujadili wengine. Bure kabisa.
 
Naiheshimu sana Marekani ila misaada yake kupitia USAID huwa ni kiini macho. Hela nyingi hurudi Marekani. Zinazobaki nchini ni kidogo. Mimi nilishawahi supply kwenye taasisi fulani maarufu hapa nchini ila kiukweli sikufurahia kabisa. Ni kwamba wakati unapewa list ya vitu vya ku-supply kuna column wamekuwekea kabisa link ya duka unaloweza kupata hivyo vitu na bei zake... maduka yapo UK na USA. Ni vitu vichache sana utanunua tofauti na hayo maduka yao. Hadi ulipwe unakuta net profit kidogo mno. Hela nyingi zinakuwa zimerudi USA. Utaishia tu kujifariji kujaza fomu fulani za hazina ya USA ili ulipwe. Kwamba hata hazina yao inakutambua. Pia USAID wanakuwa na watu wa kati. Taasisi za hapa nchini hazipati hela direct.. kunakuwa na kampuni katikati. Mambo ya ajabu sana.
 
Usipotosheka,nitakuongeza

Acha uongo.
 
Marekani inachangia kila mwaka dola milioni 500 (shilingi Trilioni 1.2) kwenye shirika la afya duniani.

mataifa mengine yana watu wengi zaidi mfano China, ina watu zaidi ya bilioni 1 inachangia Dola milioni 20 (shilingi bilioni 50) .

Marekani baada ya kuona pesa zao zinafujwa, Trump kaamua kusitisha michango.

Kelele na Lawama nyingi zimezuka baada ya Marekani kusitiha misaada kukiwa na malalamiko ya ufinyu wa bajeti.

Nchi za Afrika zimekuwa mstari wa Mbele kutoa Lawama lakini ni viongozi hao wanaolalamika wanaongoza kwa kutapanya misaada inayotolewa kila mwaka inayoishia mifukoni mwa wachache.

Sio shirika la afya tu, Kwenye ulinzi wa nchi za Ulaya (NATO) Marekani ndie anaechangia zaidi, nchi zote za ulaya zinategea kukwepa michango.
Ukizoea vya bure... Wanaolalamika hawana akili
 
Naiheshimu sana Marekani ila misaada yake kupitia USAID huwa ni kiini macho. Hela nyingi hurudi Marekani. Zinazobaki nchini ni kidogo. Mimi nilishawahi supply kwenye taasisi fulani maarufu hapa nchini ila kiukweli sikufurahia kabisa. Ni kwamba wakati unapewa list ya vitu vya ku-supply kuna column wamekuwekea kabisa link ya duka unaloweza kupata hivyo vitu na bei zake... maduka yapo UK na USA. Ni vitu vichache sana utanunua tofauti na hayo maduka yao. Hadi ulipwe unakuta net profit kidogo mno. Hela nyingi zinakuwa zimerudi USA. Utaishia tu kujifariji kujaza fomu fulani za hazina ya USA ili ulipwe. Kwamba hata hazina yao inakutambua. Pia USAID wanakuwa na watu wa kati. Taasisi za hapa nchini hazipati hela direct.. kunakuwa na kampuni katikati. Mambo ya ajabu sana.
Sawa tu, hakuna Cha bure
Kwann mtu utegemee mwanadamu wakati nchi Ina Kila kitu so ujinga huu
 
Usipotosheka,nitakuongeza

Tutapiga piga chenga lakini ukweli utabaki palepale kwamba Afrika hatuna uongozi bora na sera nzuri unaoweza kutuondoa kwenye tope hili zito tulimokwamamo.

Ukiangalia nchi kama China, Vietnam, Singapore, Thailand, Malaysia na Indonesia maendeleo yao yameletwa na uongozi bora na sera nzuri na wala siyo misaada.

Tatizo kubwa la Afrika, wanafikiri wanaweza wakaendelea kwa tumisaada wanazopewa na wazungu na kwa njia hii maendeleo wataishia kuyaona tu kwenye runinga zao kwa mabara mengine.

Tuchukulie mfano wa Tanzania, kila mwaka ripoti ya CAG inaonyesha jinsi ufisadi mkubwa unavyofanyika kwa fedha za umma japo kuna mengine ambayo hufichwa ili "kulinda heshima ya nchi", halafu bado wajinga fulani wanataka walaumu wazungu kwa kukosa kwao maendeleo.

Ikumbukwe kwamba katika Tanzania hakuna mtumishi yeyote wa serikali aliyewahi kushitakiwa kwa tuhuma za kujihusisha na ubadhirifu wa fedha za umma kwani wakurugenzi wote wa halmashauri za wilaya ni makada wa chama tawala na ni hivyo hivyo kwa wakuu wa mikoa na wilaya na watu hao ni muhimu sana kwa mikakati ya chama tawala kuendelea kubaki madarakani.

Hivyo hii ya kusema kwamba tunaibiwa na wazungu ni kisingizio feki kinachotumiwa na watawala kurubuni wananchi wengi ambao bado hawajitambui ili waamini kwamba wazungu ndio chanzo cha umaskini wao na ajabu haohao watawala huiba hela na kwenda kuzificha tena hukohuko kwa hao wazungu..😛😛😛
 
Marekani inaongoza kuiba rasilimali duniani kote,huo siyo msaada bali kidogo katika faida kubwa aibayo
🤣🤣 ukiambiwa prove wanaibaje utaweza? Si viongozi wako wanawakaribisha kwa mikono miwili kwa ku sign mikataba ya siri?
Wanawaita wawekezaji
 
Back
Top Bottom