Marekani kutoza “ushuru sawa” kuleta changamoto kubwa kwa Afrika

Marekani kutoza “ushuru sawa” kuleta changamoto kubwa kwa Afrika

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
126
Reaction score
215
Hivi karibuni serikali ya Marekani ilitangaza sera mpya ya ushuru wa forodha, na kutoza viwango sawa vya ushuru wa forodha kulingana na Marekani inavyotozwa na nchi nyingine.

Wachambuzi wengi wanaona kuwa sera hiyo inayoitwa “ushuru sawa” ya Marekani italeta athari kubwa kwa nchi zinazoendelea haswa nchi za Afrika, na kusababisha changamoto kwa maendeleo ya bara la Afrika.

Msingi wa uchumi na biashara barani Afrika ni duni, na nchi nyingi za Afrika haswa zinauza mazao na malighafi za kiasili kwa nchi nyingine Muundo huo wa kibiashara unaifanya Afrika iwe na nafasi ndogo katika biashara ya kimataifa, na sera mpya ya ushuru ya Marekani itafanya hali hiyo kuwa mbaya zaidi.

Ukweli ni kwamba sera hiyo kwa kisingizio la kuhimiza biashara yenye haki zaidi ni kitendo kingine cha Marekani cha kujilinda kibiashara dhidi ya nchi zinazoendelea.

Kwani inapuuza pengo kubwa la maendeleo kati ya nchi zinazoendelea na Marekani, na ikiwa nchi yenye nguvu kubwa zaidi ya kiuchumi duniani, Marekani kutoza ushuru sawa na nchi za Afrika ni kama Mike Tyson kupigana ngumi na mtoto mchanga.

Kama sera ya Marekani ya “ushuru sawa” ikitekelezwa, bila shaka italeta changamoto kubwa kwa uchumi wa Afrika. Bidhaa nyingi za nchi za Afrika zinazouzwa Marekani ni mazao ya kilimo na rasilimali za madini.

Bidhaa hizi zina faida ndogo, na ushuru mkubwa utasababisha moja kwa moja bidhaa za Afrika kupoteza ushindani wao wa soko. Mbali na bidhaa za kiasili, mchakato wa maendeleo ya viwanda barani Afrika pia utakabiliwa na changamoto.

Kwa mfano, sekta ya nguo nchini Ethiopia iko katika kipindi muhimu cha kustawi, na kama ikitozwa ushuru wa kiwango cha juu na Marekani, uwezo wa ushindani utapungua kwa kiasi kikubwa.

Aidha, sera mpya ya ushuru ya Marekani si kama tu itaathiri biashara ya bidhaa, bali pia itadhoofisha imani na fursa ya nchi za Afrika kushiriki katika mlolongo wa kimataifa wa viwanda.

Ili kukabiliana na sera mpya ya ushuru ya Marekani, nchi za Afrika zinapaswa kuimarisha mshikamano wa ndani. Ujenzi wa Eneo la Biashara Huria la Afrika umetoa jukwaa muhimu kwa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara wa kikanda.

Nchi za Afrika zinatakiwa kuharakisha utekelezaji wa makubaliano ya biashara huria, ili kupanua biashara ya kikanda, na kupunguza utegemezi wa masoko ya nje.

Aidha, kuimarisha ushirikiano wa nchi za Dunia ya Kusini pia ni njia muhimu kwa Afrika kukabiliana na changamoto hiyo. Mbali na hayo, nchi za Afrika zinapaswa kushiriki kwa hatua madhubuti zaidi katika mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa uchumi wa kimataifa, na kuhimiza kuanzisha utaratibu mpya wenye haki wa kibiashara duniani.

Sera mpya ya ushuru ya Marekani ni ukiukaji wa haki ya kupata maendeleo ya Afrika, nan i lazima kwa nchi za Afrika zitambue hali hiyo na kushikamana ili kukabiliana na changamoto.

Jumuiya ya kimataifa pia inapaswa kupinga kwa pamoja sera hiyo ya Marekani, ili kulinda mfumo wa biashara wa kimataifa, na kuanzisha mazingira ya haki ya maendeleo kwa nchi zinazoendelea ikiwa ni pamoja na nchi za Afrika.
 
Africa ni jehanam ndogo, matatizo yote ya dunia hii yanakuja kuangukia Africa
 
Back
Top Bottom