Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Wakati shughuli za uokoaji zikiendelea katika jengo la ghorofa 12 lililoporomoka siku ya Ijumaa nje kidogo ya mji wa Miami, Florida nchini Marekani, miili zaidi imetolewa katika kifusi cha jengo hilo.
Watu 9 waliripotiwa kufariki kufikia siku ya Jumapili, akiwamo mtu mmoja aliyefariki akiwa hospitalini, huku wengine zaidi ya 150 wakiwa hawajulikani walipo. Wengine 8 wameokolewa na wapo salama.
Marekani imeomba msaada wa wataalamu wa uokoaji kutoka Israel na Mexico baada ya shughuli za uokoaji kutatizwa na moto uliokuwa ukiwaka katikati ya kifusi siku ya Jumamosi.
Kitendawili cha jengo hilo kuporomoka bado hakijatenduliwa. Vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kuwa mwaka 2018, wahandisi walionya nyufa katika msingi wa jengo hilo na kuwa lilihitaji ukarabati mkubwa. Ripoti hiyo ilionesha pia uwepo wa nyufa katika nguzo na kuta za eneo la kupaki magari katika jengo hilo.
Zikiwa zimepita zaidi ya saa 80 tangu kuporomoka kwa jengo hulo, waokoaji wanasema bado kuna matumaini ya kuwapata wahanga wakiwa hai. Wakati huo, familia na marafiki wa wakazi wa jengo hilo wanasubiri kwa hamu taarifa zozote kutoka kwa timu za waokoaji. Baadhi yao wametoa sampuli za vinasaba (DNA) ili kuwatambua kwa urahisi watakaookolewa.
Mmiliki wa jengo hilo, Erick de Moursa anasema alipaswa kuwepo nyumbani wakati jengo hilo lilipoporomoka, lakini alishawishiwa na mpenzi wake kubaki naye usiku, umbali wa takriban kilomita 3 kutoka eneo jengo lililoporomoka, na kuyaokoa maisha yake.
“Ni Mungu tu. Kwangu mimi huu ni muujiza,” raia huyo wa Brazil aliliambia Shirika la Habari la Reuters.
Chanzo: Al Jazeera
Mwanamke akisali katika ufukwe wa Miami, Florida wakati waokoaji wakiendelea kutafuta miili katika kifusi cha jengo hilo | Picha: Reuters