Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Ila hapa duniani kuna watu na viatu kwa kweli!
Sasa mtu anatumwa na halmashauri yake ya kichwa anaenda kuwasha moto duh hii ni balaa tupu. Pole zao wote walipata janga hili kubwa.
=====================
Idara ya Polisi ya Los Angeles (LAPD) imesema inamshikilia mtu mmoja anayedaiwa kusababisha moto mkali uliochoma nyumba zaidi ya 10,000 na kuua watu 10 nchini Marekani.
Moto huo ulioanza usiku wa kuamkia Januari 9, 2025 umeteketeza nyumba za kifahari za mbele ya bahari.
Ofisa mkuu wa LAPD, Charles Dinsel ameuambia mtandao wa NewsNation jana Januari 9, kwamba mshukiwa mmoja yuko chini ya ulinzi, akihisiwa kusababisha moto huo kwa makusudi.
Soma Pia: Marekani: Moto Mkali Wateketeza Ekari 3,000 na Kuwafurusha Maelfu ya Watu Los Angeles
"Baada ya dakika 20 hadi 30, mshukiwa alikamatwa katika eneo la Woodland Hills na wananchi. Hili linachunguzwa kama uhalifu," amesema Dinsel.
Ofisa huyo alipotakiwa kueleza moja kwa moja kama moto huo uliwashwa kwa makusudi, "Kwa sasa, tunaamini hivyo. Ndiyo."