Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Kesi ya Mwanamke aitwae Sarah Boone (46) wa Florida Nchini Marekani anayetuhumiwa kwa kusababisha kifo cha Mpenzi wake ( Jorge Torres 42) kwa kumfungia kwenye sanduku la nguo na kumsababishia kukosa hewa kulikosababisha kifo chake mwaka 2020, inatarajiwa kusikilizwa wiki ijayo baada ya kusogezwa mbele kufuatia Jimbo la Florida kukumbwa na Kimbunga Milton.
Akisimulia kilichotokea siku ya tukio, Sarah amedai kuwa walikuwa wakicheza mchezo wa kujificha na kutafutana ( hide and seek ) wakiwa wamelewa ambapo alipatwa na usingizi baada ya kumfungia Jorge ndani ya sanduku hilo na alipoamka asubuhi akakuta Mpenzi wake huyo amefariki.
Licha ya ushahidi wa video iliyopatikana kwenye simu ya Sarah kuonesha mazungumzo yao kabla ya kifo cha Jorge ambayo Sarah amesikika akicheka na kumkejeli Jorge pale alipomwaambia hawezi kupumua ndani ya sanduku hilo, Sarah amekataa ombi la Waendesha mashtaka lililomtaka akiri kosa ili kupokea kifungo cha miaka 15 jela kwa kukiri kosa la kuua bila kukusudia.
Katika video hiyo Sarah amesikika akimfokea Jorge baada ya kusema anashindwa kupumua ambapo Sarah alinukuliwa akimuambia “katika vitu vyote ulivyonifanyia, hiyo ni juu yako.... na hivyo ndivyo ambavyo mimi hujusikia unavyokuwa umechepuka”