Marekani, Uingereza & Norway zimeitaka Sudan Kusini kuunda serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa kabla ya Februari 22, 2020 ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya amani. Mambo yanayoleta mvutano ni: majimbo mangapi yawepo na kuunganishwa kwa wanajeshi 83,000 kutoka vikundi mbalimbali.