Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,434
- 27,177
Naam FIFA imeifungiaUrusi ifungiwe na Marekani kucheza kombe la Dunia? Hawa ku qualify
soma aya ya kwanza umeandika nnSafonov wa PSG alyewanyima uefa ni mrusi
Baada ya kuchukua ubingwa alikuwa analia tu familia yake hairuhusiwi kuingia ulaya so alkuwa mpweke wenzie wakat wapo na familia zao wakichukua snap
Sio FIFA tu, dunia nzima imewekwa mfukoni na Marekani.Ila FIFA sasa hivi ni kama imewekwa mfukoni na Marekani
Kwani Marekani ina kosa gani kwa sababu kisheria kila nchi ina haki ya kujilinda kiusalama.FIFA iko hivyo miaka zote, iinatumika kisiasa kukandamiza mataifa mengine huku wakijifanya siasa hairuhusiwi kwenye soka. Israel imevamia Palestina, inaua, inateka na kuua mamlioni ya ya raia lakini haijawahi kufungiwa. Mashindano yakifanyike nchi zingine wakizingua wanachapwa faini haraka sana au kufungiwa kama Indonesia ila Marekani huoni hata tamko tu
Haikua na mpango wa kufatilia hao wazamiaji? Suala la mashabiki kuja kuzishangilia timu zao mbona ilo sio jambo geni. Yule refa msomali hata angezamia mbona kumpata ingekua rahisi tuKwani Marekani ina kosa gani kwa sababu kisheria kila nchi ina haki ya kujilinda kiusalama.
Na shida ya wanaoenda kuangalia mashindano ya kombe la dunia ni kwamba wengine wakifika huko hawataki kurejea makwao na badala yake watataka wazamie ili kukimbia shida katika nchi zao na Marekani wanalifahamu hilo.
Kila mwaka mamilioni kwa mamilioni ya watu hutafuta viza ya Marekani ili wakazamie huko.
Ukifungiwa na Marekani umefungiwa Duni nzimaKama USA imemrudisha refa wa Somalia, basi ile ni isue ndogo sana kwa Marekani, hili la Urusi Gen Z na millenia hamjui.
Urusi haishiriki Kombe la Dunia la 2026 kwa sababu FIFA iliweka kizuizi rasmi kinachozuia timu hiyo kushiriki katika mashindano yake yote tangu mwezi Februari 2022.
Hali hii ilitokana na uvamizi wa kijeshi wa nchi hiyo nchini Ukraine, ambao ulisababisha mashirikisho ya soka duniani kuitenga nchi hiyo kisiasa na kimichezo.
Kutokana na adhabu hiyo, timu ya taifa ya Urusi haikuruhusiwa kushiriki kwenye mechi za mchujo (qualifiers) za kuwania nafasi za kufuzu fainali hizi za 2026 zinazoandaliwa na nchi za Marekani, Mexico, na Canada.
Pia, Soma:
Hivi sasa (2026), hakuna wachezaji kutoka nchi ya Urusi wanaocheza kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) wala Ligi Kuu ya Hispania (La Liga). Kutokana na vikwazo vya kisiasa na mizozo ya kimataifa, wachezaji wengi wa kulipwa wa Urusi wanasakata soka lao katika Ligi Kuu ya nchini mwao (RPL) au ligi nyingine barani Ulaya kama Ufaransa (Ligue 1].
- Mataifa matano Afrika yanapaswa kuilipa Marekani dola 15,000 kwa shabiki mmoja Kombe la Dunia
- Mwamuzi wa Somalia, Omar Artan, azuiwa kuingia Marekani, kuchezesha Kombe la Dunia 2026
Mijadala mingine kuhusu Kombe la Dunia;
- Trump: Kwa kweli ‘sijali’ kama Iran itashiriki Kombe la Dunia 2026
- Orodha ya Waamuzi wa Afrika watakaochezesha mechi za FIFA World Cup 2026
- FIFA yakataa ombi la Iran la kucheza mechi za Kombe la Dunia nje ya Marekani
- DR Congo yaiomba FIFA kurejesha Fedha za Tiketi za Kombe la Dunia 2026 kutokana na Vikwazo vya Ebola vilivyowekwa na Marekani
Marekani ni special case nchi zingine hizo hakuna watu wanaopenda kuzamiamo.Haikua na mpango wa kufatilia hao wazamiaji? Suala la mashabiki kuja kuzishangilia timu zao mbona ilo sio jambo geni. Yule refa msomali hata angezamia mbona kumpata ingekua rahisi tu
Walitakiwa kuongeza ulinzi sio kuzuia watu wasiingie nchini mwao. Ni matumaini yangu uko mbeleni mwenyeji mwingine akipiga hizi marufuku za timu, marefa na mashabiki kuingia kwenye nchi yake nae pia ataelewekaMarekani ni special case nchi zingine hizo hakuna watu wanaopenda kuzamiamo.
Hatari sana