Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Kiongozi wa Wademocrat katika Baraza la Seneti nchini Marekani Chuck Schumer leo ametoa wito kwa mamlaka za nchi hiyo kukomesha mauzo ya vitambulisho bandia vya chanjo ya Covid-19 vinavyouzwa mtandaoni.
Wito wa Schumer unafuatia ripoti za shirika la habari la Associated Press zilizofichua jinsi watu wananunua kadi za chanjo mtandaoni.
Hali hiyo imezua wasiwasi mkubwa miongoni mwa maafisa wa shule na vyuo vikuu nchini Marekani vinavyohitaji uthibitisho wa mtu kuchanjwa dhidi ya Covid-19 kabla ya kuruhusiwa kuhudhuria masomo darasani.
Schumer amezitaka idara za ulinzi wa mipaka, shirika la upelelezi la FBI kwa kushirikiana na wizara ya afya kufanya operesheni ya pamoja kukomesha kadi bandia. Amezitaka pia mamlaka za serikali kuu kuendesha kampeni ya kuwakumbusha raia kwamba kugushi kadi za chanjo kunaweza kupeleka gerezani.