Marekani: Watu 70 wafariki kutokana na Kimbunga

Marekani: Watu 70 wafariki kutokana na Kimbunga

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Kimbunga Tornado kilicho tawanyika na kuyakumba maeneo ya majimbo sita tofauti nchini Marekani kimesababisha watu zaidi ya 70 kupoteza maisha.

Akithibitisha athari hiyo Gavana wa jimbo la Kentucky amesema pamoja na vifo vya idadi hiyo ya watu wanaopindukia 70 upo uwezekano wa idadi hiyo kuongezeka zaidi. Amesema kimbuka hicho pia kimefanya uharibfu mkubwa wa makazi.

Gavana Andy Beshear amesema tatizo hilo limelikumba eneo la umbali wa maili 20 kwa Kentucky pekee na idadi ya vifo inaweza kuzidi 100 kwa rekodi za majimbo mengine 10 zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi gavana hiyo amesema kimbunga hicho, tonardo, kimeingia katika rekodi ya kuwa chenye uharibifu zaidi. Kimbunga kimekikumba kiwanda cha mishumaa cha Kentucky, eneo la kampuni ya Amazon jimboni Illios na nyumba ya wazee ya Arkansas.

Gavana Beshear aliongeza kwa kusema takribani watu 110 walikuwa katika moja ya kiwanda cha jimbo hilo wakati kimbunga hicho kilipozuka. Awali Asubuhi maafisa walithibitisha kutoka vifo vya watu 18, lakini baadae Beshear alisema idadi ya vifo inaweuza kuwa imeongezeka.
 
Waliwezaje kuto forecast uwepo wa tornado yenye ukubwa wa madhara tajwa?

Ukichukulia jimbo lililotajwa hapo ni moja ya majimbo yanagongwa sana na vimbunga...
 
Ingekuwa bongo lazima lawama wangepewa wakile chama kwamba miaka 60 bado miundombinu mibovu kweli bongo nyoso.[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom