Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Marekani imeuonya Umoja wa Mataifa kuwa ina habari kwamba Urusi ina orodha ya raia wa Ukraine wanaopaswa kuuawa ama kuweka kwenye kambi za mateso iwapo uvamizi dhidi ya Ukraine utatokea.
Haya ni kwa mujibu wa barua iliyotumwa kwa Mkuu wa Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa, Michelle Bachelet, na nakala yake kupatikana na shirika la habari la AFP. Barua hiyo imesema kwamba Marekani ina taarifa za kuaminika zinazoonyesha kwamba vikosi vya Urusi vinandaa orodha hiyo na wana taarifa pia kuwa vikosi vya Urusi vinaweza kuchukuwa hatua za hatari kutawanya maandamano ya amani au upinzani unaojulikana kutoka kwa raia.
Waraka huo, uliotiwa saini na Bathsheba Nell Crocker, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa mjini Geneva, unaonya kuwa uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine unaweza kuleta dhuluma kama vile utekaji nyara au mateso, na unaweza kuwalenga wapinzani wa kisiasa na watu wa dini na makabila ya wachache, miongoni mwa mengine. Moscow inakanusha kuwa ina mpango wa kushambulia Ukraine lakini inatafuta hakikisho kwamba Ukraine haitajiunga na NATO.
DW Swahili