Marekani yaendelea kujihisi upweke katika jukwaa la jumuiya ya kimataifa

Marekani yaendelea kujihisi upweke katika jukwaa la jumuiya ya kimataifa

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
TIM图片20200916080501.jpg

Hivi majuzi, Umoja wa Mataifa umepitisha azimio moja kuhusu maambukizi ya virusi vya Corona kwa kura 169 za ndiyo dhidi ya kura 2 za hapana. Marekani na Israel zimekuwa nchi pekee zilizopiga kura za hapana. Marekani inatia mashaka kuhusu kama Shirika la Afya Duniani WHO linatoa mchango katika kuratibu mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona duniani au la, lakini mashaka hayo hayajatambuliwa na jumuiya ya kimataifa.

Tukio hilo si la pekee, katika wiki tatu zilizopita Marekani ilishindwa kwa mara ya tatu katika Umoja wa Mataifa. Agosti 21, Marekani ililitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuzindua mfumo wa kurejesha vikwazo dhidi ya Iran, lakini nchi wanachama 13 kati ya 15 zilipinga matakwa hayo. Agosti 24, bila kujali shinikizo na tishio la Marekani, nchi zilizojiunga na makubaliano ya sheria ya bahari ya Umoja wa Mataifa zimemchagua Bw. Duan Jielong aliyependekezwa na serikali ya China kuwa jaji mkuu wa mahakama ya sheria ya kimataifa.

Wachambuzi wanaona kuwa Marekani sasa inajihisi upweke katika jumuiya ya kimataifa, upweke ambao haikuwahi kuuona kabla ya hapo. Kushindwa kwa mara ya tatu kwa Marekani katika Umoja wa Mataifa ndani ya wiki tatu kumeonesha mambo matatu.

La kwanza, Marekani imekuwa mvunjaji mkubwa zaidi wa utaratibu wa kimataifa uliopo hivi sasa. Baada ya vita vya pili vya dunia, Marekani ilikuwa nchi iliyoongoza kujenga utaratibu wa dunia. Lakini miaka ya hivi karibuni, Marekani inatekeleza kipaumbele cha Marekani, na kujitoa kwenye mifumo mingi ya pande nyingi, huku ikileta tishio kubwa kwenye utaratibu wa kimataifa na utulivu wa dunia. Ukweli ni kwamba idadi ya makubaliano ya kimataifa iliyojitoa serikali ya awamu hii ya Marekani imekuwa kubwa zaidi katika historia ya nchi hiyo ikilinganishwa na serikali ya awamu yoyote.

La pili, umwamba wa Marekani sasa unaepingwa na nchi mbalimbali duniani. Kutokana na sera ya “Kipaumbele cha Marekani”, Marekani imepoteza uwezo wake wa kuiongoza jumuiya ya kimataifa. Hasa katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona, Marekani ikiwa nchi inayoathiriwa vibaya zaidi na maambukizi hayo, serikali yake imepoteza hadhi ya kuwa kinara duniani katika shughuli mbalimbali za kimataifa. Hivyo, wachambuzi wanaona kuwa dunia ya ncha moja ya Marekani hatimaye inaelekea kwisha.

La tatu, ingawa Marekani imeshindwa mara nyingi katika ajenda nyingi za kimataifa, lakini bado inaendelea kwenda kinyume na makubaliano ya kimataifa. Nchi hiyo bado haijatambua umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika ulinzi wa amani na haki. Inakadiriwa kuwa, katika siku za baadaye, Marekani italeta changamoto nyingi zaidi kwenye utaratibu wa kimataifa.

Dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayakuwahi kuonekana katika miongo mingi, umwamba na mfumo wa upande mmoja havitaondoka kwa hiari katika jukwaa la kimataifa. Jumuiya ya kimataifa inatakiwa kushikamana, kuimarisha ushirikiano wa mifumo ya pande nyingi, kufanya mageuzi na kuboresha mfumo wa utawala wa dunia, ili kuhimiza ukuaji wa uchumi wa dunia na kulinda haki na usawa wa kimataifa.
 
Kukomesha ufedhuli wa Merikani - binafsi napendekeza makao makuu ya Umoja was Mataifa uhamishiwe the Hague Uswizi pamoja na agencies zake.
 
Kwenye kura kila mtu ana haki ya kupiga kulingana na anavyoona inafaa, hivyo hamna kitu cha ajabu hapo. Ni kuanzisha tu mada isiyokuwa na maana.
 
Back
Top Bottom