At the end Marekani itapeleka silaha Georgia.
Marekani ina Rais wake, ila siasa za nchi hiyo, na hivyo maamuzi mengi, yanasukumwa na interest groups nyingi tu. Makampuni ya kutengeneza na kuuza silaha kama Boeing, Lockheed, MD etc. yanapenda wapate soko zaidi, hivyo watashinikiza wawakilishi wao (Senators & Congressmen) washawishi Serikali ya Marekani iiuzie Georgia silaha ili wao wapate soko na pesa.
Urusi nayo itachangia Georgia iuziwe silaha, kwa kuwa Urusi imekuwa dhaifu kutetea misimamo yake hata pale inapochokozwa na vibaraka wa Marekani. Mfano vita vya Georgia vilianza pale majeshi ya Georgia yaliposhambulia majeshi ya kulinda amani ya Urusi na kukiuka makubaliano ya amani kati ya Urusi, Georgia na wapinzani wa Saakashvili. Georgia alivizia siku ya kuanza michezo ya Olimpiki ya Beijing kwa kuwa Putin alikuwa China. Marekani wa nchi za Magharibi wanamuona Medvedev kama mnyonge fulani hivi. Na hiyo ni kweli.
Kwa kuwa Saakashvili wa Georgia ni kibaraka wa Marekani, hajapelekwa ICC kule The Hague. Ni Mahakama ya kisiasa inayoshtaki tu maadui wa kisiasa wa Marekani (Milosevic, Taylor, Al-Bashir). Marafiki wa Marekani (Sharon, Olmert, Saakashvili), na wamarekani kama George W. Bush, Dick Cheney, Donald Rumsfeld hawakamatwi.
Marekani inapenda sana kutumia kisingizio cha 'demokrasia' kutaka Serikali ambazo si marafiki wala vibaraka wake ziondolewe madarakani, na hapohapo haitaki uchaguzi wa haki kwenye nchi ambazo inaelekea Serikali za vibaraka wake zitashindwa kwenye uchaguzi wa haki (mfano Misri kuna uchaguzi feki na nchi nyingine za Mashariki ya Kati huwa hakuna uchaguzi. Hamas ilishinda uchaguzi Palestina, nchi za magharibi wakakataa kuitambua na wakamwambia Mahmoud Abbas ang'ang'anie madarakani hadi leo yupo).
Rais Medvedev wa Urusi alifanya upuuzi alipokubaliana na Obama kuwa Urusi na Marekani zipunguze idadi ya makombora yao ya nyuklia hadi yabaki 1,500 kwa kila mmoja. Hivi sasa Urusi inayo 2,800 na Marekani 2,200.
Kumbuka kuwa Kamanda Mkuu wa Majeshi ya NATO always ni Mmarekani anayeteuliwa na Rais wa Marekani. Hivyo majeshi ya nchi za NATO yako chini ya Marekani, na marais wa Ukraine na Georgia wanatamani kujiunga NATO. Hivyo Urusi itakuwa imezungukwa.
Kama Urusi ingekuwa na strong responses, nchi za magharibi zingerudisha heshima. Kumbuka comments za western politicians na media kuwa hawakutegemea kuwa Urusi ingezuia majeshi ya Georgia. Wamefikia kuidharau kiasi hicho.
Toka Umoja wa Sovieti usambaratike, Marekani imekuwa ikikiuka makubaliano mengi tu, kama vile kutoeneza majeshi ya NATO eneo la Ujerumani Mashariki (ikaeneza), kutoruhusu nchi za zamani za WARSAW PACT kujiunga na NATO (ikazialika na zikajiunga), kutoruhusu nchi zilizokuwa zukiunda Umoja wa Sovieti kujiunga na NATO (imesema zina 'haki' ya kujiunga). Ni Urusi yenyewe tu ambayo imeambiwa haiwezi kuruhusiwa kujiunga. Sababu iko wazi.
Kule Umoja wa Mataifa kwa mfano, Urusi ilitakiwa kutumia kura yake ya VETO kupinga vikwazo haramu dhidi ya Iran na Korea Kaskazini, kama ambavyo Marekani siku zote huwa inapiga kura ya VETO kupinga maamuzi dhidi ya Israel ambayo inatengeneza silaha za nyuklia Urusi haikufanya leo.
Kutokana na Urusi kuonyesha response dhaifu, Marekani itauza silaha popote inapotaka, hata nchi jirani na adui na Urusi. Hii ni mpaka hapo Urusi itakapobadilika na kuwa inakomaa kama China inavyojaribu.