#COVID19 Marekani yaiweka Tanzania katika orodha ya nchi hatari kusafiri

#COVID19 Marekani yaiweka Tanzania katika orodha ya nchi hatari kusafiri

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Marekani imeweka Tanzania katika orodha yake ya nchi hatari kusafiri, ikitoa ushauri kwa raia wake kutosafiri katika taifa hilo.

Kituo cha kudhibiti magonjwa nchini Marekani (CDC) imeweka Tanzania katika orodha ya nchi hatari kusafiri.

Kituo hicho kimesema ni vyema kutosafiri katika taifa hilo na kama kuna ulazima basi mtu amepata chanjo kamili dhidi ya corona.

Aidha wamesema, "hali ya sasa nchini Tanzania, hata wasafiri walio na chanjo kamili wanaweza kuwa katika hatari ya kupata na kueneza virusi vipya vya corona" CDC imesema.

Siku ya Jumapili, taarifa zilienea mitandaoni kuwa msafiri kutoka Tanzania alipimwa na kukutwa na aina mpya ya virusi vya corona- Omicron huko New Delhi, India, na kusababisha mamlaka 'kuanza uchunguzi'.

Licha ya tahadhari za mara kwa mara kutoka kwa Wizara ya Afya ya Tanzania, uzingatiaji wa umma kwa hatua za kuzuia Covid-19 bado ukochini, Ubalozi wa Marekani umesema.

BBC Swahili
 
Kuna homa zinawapiga watu mtaani kinomanoma.

Nadhani tungekuwa serious na upimaji, Tz tungekuwa tuna the most advanced corona virus than Omicron.

Watu karibu kila mtaa wanaumwa na dalili ni zilezile ila wakienda kupimwa hamna ugonjwa wowote.
 
Kuna homa zinawapiga watu mtaani kinomanoma.

Nadhani tungekuwa serious na upimaji, Tz tungekuwa tuna the most advanced corona virus than Omicron.

Watu karibu kila mtaa wanaumwa na dalili ni zilezile ila wakienda kupimwa hamna ugonjwa wowote.
Duh kirusi itakua kimerudi kwa kasi kubwa sana mkuu
 
Vipi wao wenyewe hawajajiweka kwenye list?
 
Yani mtanzania amegundulika huko lakini walio mgundua hawajaambukizwa!!!!
 
-Siku zote shetani hafurahii kumuona binadamu anaishi kwa amani,anatamani binadamu awe na hofu ili aweze kumtawala.(Ni vizuri Virusi vyote viachiwe tu huko vilikojificha,Tusitishane ukichanja unatishiwa chanjo haijakamilika , usipochanja unatishwa)

-Kipaumbele chetu ni maji na umeme wa uhakika,Milo mitatu kwa siku,barabara zinazopitika misimu yote, hospitali zenye bima zinatoa dawa na huduma salama,elimu inayokidhi kujiajiri na kuajiriwa.
(Tanzania ya viwanda inawezekana penye umeme wa uhakika)

-Mtizamo wangu tukimaliza vipaumbele hivyo tuanze kupromote Corona Kama Marekani.
 
Wao wako salama kiasi gani,mbona tunaona wanaendelea kujazana kwenye maviwanja yao ya mpira bila hata ya kuvaa barakoa...?
 
Back
Top Bottom