Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Awali, msemaji wa NASA Faith Marco alilalamika kwamba China inashirikiana na Ufaransa, Italia, Pakistani na Shirika la Anga za juu la Ulaya kutekeleza mradi wa kukusanya sampuli kutoka upande wa mbali wa Mwezi, lakini haikuialika NASA kufanya hivyo, na hata sasa haiko tayari kushirikiana na Marekani kutafiti sampuli ya Mwezi.
Kuhusu suala hilo, jibu la Wizara ya Mambo ya Nje ya China limekuwa rahisi na la wazi, China siku zote inapenda kushirikiana na Marekani katika utafiti wa anga za juu, lakini labda Marekani imesahau kifungu chake cha Wolf, ambacho kinapiga marufuku mashirika yoyote ya nchi hiyo kushirikiana na China katika utafiti wa anga za juu. Naye naibu mkuu wa Shirika la Anga za Juu la China Bian Zhigang pia amesema kizuizi kikuu dhidi ya ushirikiano wa China na Marekani katika utafiti wa anga za juu ni Kifungu cha Wolf, kama Marekani ikitaka kushirikiana na China, ni lazima iondoke kizuizi hicho.
Mwaka 1999, Marekani ilitoa ripoti ya Cox, ikidai China “kuiba” teknolojia ya anga za juu ya Marekani, na kuyataka mashirika yake na hata ya nchi nyingine kutoiruhusu China kurusha roketi zao, ili kuzuia maendeleo ya teknolojia ya anga za juu ya China. Baadaye, iliona kwamba hatua hiyo haitoshi, na kuanza kutekeleza Kifungu cha Wolf mwaka 2011, ambacho kilikataza kabisa NASA kufanya mawasiliano na ushirikiano wa aina yoyote na China.
Hata hivyo, hatua hizo ilishindwa kuzuia maendeleo ya sayansi na teknolojia ya anga za juu ya China. Tangu Marekani ianzishe Kifungu cha Wolf, China imetekeleza kwa mafanikio miradi mikubwa mbalimbali ya anga za juu kama vile kujenga kituo cha anga za juu na kuchunguza sayari za Mwezi na Mars. Hivi karibuni chombo cha Chang'e No. 6 kilifika upande mbali wa Mwezi, na kurudi ikichukua sampuli ya huko. Hii ni kazi ya upainia katika historia ya binadamu. Kama ripoti ya CNN ilivyosema, China sasa ina kitu ambacho hakuna mtu mwingine aliyewahi kuwa nacho, yaani sampuli ya mawe na udongo kutoka upande mbali wa Mwezi. Ikilinganishwa na sampuli zilizopatikana zamani kwenye upande wa mbele wa Mwezi, sampuli hiyo ni muhimu kwa binadamu kuelewa muundo wa Mwezi mzima, na hata historia ya mabadiliko ya mfumo wa jua. Bila shaka Marekani inatamani sana sampuli hiyo, lakini inakwamishwa na Kifungu cha Wolf.
Katika miaka ya hivi karibuni, Marekani imezidi kujaribu kuzuia maendeleo ya teknolojia za juu za China, na kuweka vikwazo mbalimbali. Lakini kama teknolojia ya anga za juu, kitendo hicho hakiwezi kuzuia maendeleo ya China hata kidogo, kinyume chake, mara kwa mara Marekani inajidhuru mwenyewe. Ushirikiano huleta mafanikio ya pamoja, huku ubinafsi ukileta hasara. Huu ni ukweli.