mimi ni mwanafunzi, mambo mengi ninayoyasoma humu yanapita uwezo wangu, bado sijafikia kiwango . Lakini katika kujifunza kwangu nilielewa kuwa mambo ya ndani tuyatengeneze wenyewe sio kungojea kuambiwa na nchi nyingine , ndiyo maana tunataka uhuru , uhuru ni wa sisi wa tanzania kujiamulia mambo yanayotuhusu. Balozi Green ni nani hadi tunaanza kumtukuza? hapa JF yameshasemwa hayo yote anayoyaimba Balozi Green na hata mazuri zaidi. Je Balozi wetu angesema chochote cha kuishauri Marekani jinsi ya kutatua matatizo yao, unadhani angeshangiliwa? ...... Tanzania tumepiga hatua kubwa ukiangalia mambo yanavyochunguzwa na vigogo wanavyobanwa. sisi tuendelee na in case tumesahau, mapinduzi hayachukui dakika moja, yanaanza mbali, na so far ninaamini tunaenda kasi sana na mwisho wake ni mzuri tu. Watanzania - walala hoi wanaamka na kutaka uwajibikaji wa hali ya juu. JF tuendelee kuyaanika mabaya , tuendelee kuyajadili na kutoa maoni ya jinsi ya kukabiliana nayo, tutafika tu.
naendelea kujifunza