Marekani yamshukia Raila, yataka Serikali na wapinzani kuzungumza

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Serikali ya Marekani imesema kuwa imesikitishwa na hatua ya kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ya kujiapisha Jumanne wiki hii.

Aidha katika hatua nyingine, Marekani imeituhumu serikali hiyo kwa kufungia vituo vinne vya habari nchini humo ambavyo viliadhibiwa baada ya kurusha matangazo ya moja kwa moja hafla ya uapisho wa kiongozi huyo wa upinzani.

Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema kuwa taifa hilo linaamini mizozo yoyote ile inafaa kutatuliwa kwa njia stahiki za kisheria.

“Tunakataa vitendo vyovyote ambavyo vinahujumu Katiba ya Kenya na utawala wa sheria. Uhuru Kenyatta alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Oktoba 26, 2017 katika uchaguzi ambao uliidhinishwa na Mahakama ya Juu,” taarifa hiyo iliyotumwa na msemaji wa wizara hiyo Hearther Nauerth imesema.

Hata hivyo, Marekani imewahimiza viongozi wa kisiasa nchini Kenya kufanya mazungumzo kwa lengo la kuimarisha uwiano na utengamano na kutatua matatizo ya muda mrefu nchini humo.

Chanzo: BBC Swahili
 
Rais Uhuru Kenyatta keshakataa hii kitu siku nyingi sana, anasema hakuna serikali ya "nusu mkate" nafikiri hata "robo mkate" hakuna. Maana yake anataka upinzani ukae pembeni uangalie jinsi serikali ya Jubilee inavyopepea kwenye sgr ya Mombasa - Nairobi.
 
Serikali ya Marekani imesema imesikitishwa na hatua ya kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ya kujiapisha Jumanne wiki hii.
Marekani pia imeishutumu serikali kwa kufungia vituo vinne vya habari nchini humo ambavyo viliadhibiwa baada ya kupeperusha moja kwa moja hafla hiyo ya upinzani.
Umoja wa Afrika na Muungano wa Ulaya pia wameshutumu hatua hiyo ya Bw Odinga.
Kupitia taarifa, wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema taifa hilo linaamini mizozo yoyote ile inafaa kutatuliwa kwa njia zifaazo kisheria.
"Tunakataa vitendo vyovyote ambavyo vinahujumu Katiba ya Kenya na utawala wa sheria. Uhuru Kenya alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya mnamo Oktoba 26, 2017 katika uchaguzi ambao uliidhinishwa na Mahakama ya Juu," taarifa hiyo iliyotumwa na msemaji wa wizara hiyo Hearther Nauerth imesema.
"Umoja wa Afrika unakataa vitendo vyote amabvyo vinahujumu mfumo wa kikatiba na utawala wa sheria. Mwenyekiti wa Tume (Moussa Faki Mahamat) anatoa wito kwawahusika wote kujiepusha na vitendo kama hivyo ambavyo pia vinatia hatarini uthabiti wa kisiasa Kenya," taarifa ya Tume ya Umoja wa Afrika imesema.
Chanzo: BBC
 
Ngoja tufunge mipaka kabisa Kati ya Kenya na Tanzania.

Halafu , marafiki tu ndiyo wanaruhuswa kuingia Tanzania pale mtakapo chapana...
Nadhani mnaelewa hii lugha eeeh!!!
 
Hawa marekani waache kushobokea ya watu..wenye nchi hawana shida na hivyo viapo wenyewe walio maili zaidi ya 10k kutoka kenya ndo wanajifanya wanawashwa washwa sana
 
Vile wanaona msimamizi wa mali zao anaelekea kushidwa linda mali hizo, ndiposa wanyanyua midomo zao! Wa kwende huko!! Hatuwasikizi tena.
 
Naanza kumwogopa Laila...nilikuwa namchukulia poa...yumkini yupo level nyingine kisiasa
 

Wafuate mfano wa Tanzania kwani Mhe Lowassa licha ya kupata kura nyingi hajangangana kupewa nusu mkate, chama chake kinangoja mpaka 2020 na Mhe Raila asubiri mpaka 2022 ni vema aache serikali ihudumie wananchi. Kama hataki, sheria zipo, weka ndani kwani mtu mmoja haiwezekani aendelee kuchochea fujo, vurugu, raia wa kawaida kufa kwa sababu ya tamaa ya madaraka ya viongozi wachache wa siasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…