Marekani yapeleka chuki ya dhidi ya Russia kwenye mkutano wa kundi la nchi 20

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111380528890.jpg

Fadhili Mpunji

Mgogoro wa Ukraine unaendelea kufichua hali ya umwamba kwenye siasa za kimataifa, ambao sasa umefikia hatua ya nchi moja kuzilazimisha nchi nyingine kufuata msimamo wake, na kufanya vitendo vya kulenga nchi zisizokubaliana na hali hiyo. Kwa baadhi ya nchi za magharibi, dhana kuhusu uhuru wa nchi kufanya maamuzi kwa mujibu wa maslahi yake na mazingira yake, ambayo ni msingi wa uhusiano wa kimataifa inawezekana tu na inaheshimiwa pale maamuzi hayo yanapokuwa na manufaa kwa nchi za magharibi. Vinginevyo dhana hiyo ni maneno matupu.

Hivi karibuni Marekani na washirika wake wamekuwa wakitumia njia mbalimbali za kutoa shinikizo kupinga operesheni ya Russia nchini Ukraine, ikiwa ni pamoja na kutoka nje kwenye mkutano wa kundi la G20 kuonyesha kuisusia Russia, na kuweka msururu wa vikwazo fedha ili kudhoofisha uwezo wa Russia kuendesha operesheni yake. Licha ya kuwa jambo hili si la kufurahisha, lakini wachambuzi wa maswala ya kisiasa wanaona ni moja ya njia zinazotumika kwenye migogoro. Lakini kinacholeta ukakasi ni pale ambapo Marekani na washirika wake wanajaribu kuzilazimisha nchi nyingine zifuate msimamo wao, au kuzitaka ziitii na kuchukua hatua kama inavyotaka Marekani, bila kujali maoni ya nchi hizo kuhusu mgogoro wenyewe.

Mara nyingi China imekuwa ikirudia mara kwa mara msimamo wake wa siku nyingi wa kutopendelea upande wowote kwenye migogoro, na kuhimiza njia ya mazungumzo kuwa ufumbuzi sahihi wa mgogoro huo. Nchi kadhaa ikiwa ni pamoja na nchi za Afrika, pia zimeonesha msimamo kama huo kwenye mgogoro wa Ukraine. Lakini Marekani imeanza kuipaka matope China kwa kuendelea na urafiki wa muda mrefu na Russia katika kipindi hiki ambapo kuna mgogoro na Ukraine, kwani inahisi au inahofu kuwa urafiki huu unaweza kuikwamisha kwenye malengo yake. Kwa hiyo inailazimisha China kuipinga Russia, na pale China inapokataa kufanya hivyo au inapokuwa kimya, inaitaja China kuwa ni “msaidizi wa Russia”. Wachambuzi wa maswala ya kimataifa wanaona hali hii si ya ajabu, bali ni janja ya siku zote ya Marekani yenye malengo mawili.

Lengo la kwanza ni kutaka nchi za Ulaya ambazo ni washirika wa Marekani ziichukie China. Ukweli ni kwamba vikwazo vilivyowekwa na Marekani na nchi za magharibi dhidi ya Russia, licha ya kuathiri uchumi wa Russia pia vimekuwa ni mwiba mchungu kwa nchi za Ulaya ambazo zimeanza kushuhudia kupanda kwa gharama za maisha. Inachofanya Marekani ni kutaka nchi za Ulaya zione kuwa uchungu huo unaotokana na kukatishwa kwa biashara ya mafuta na gesi na Russia, unatokana na baadhi ya nchi kutoipinga Russia, na haukusababishwa na Marekani. Kwa hiyo inachofanya Marekani ni kuzusha “maadui wa kufikirika” kuwa ndio chanzo cha taabu za watu wa Ulaya, na kujaribu kuwaaminisha watu wa Ulaya kuwa sio vikwazo vilivyowekwa na Marekani na washirika wake, bali ni China na Russia ndio sababu ya taabu zao.

Profesa Diao Daming wa Chuo Kikuu cha Renmin cha Beijing, amesema toka mwanzo Marekani ilikuwa inaweka mazingira ya kuishinikiza China ijiunge kwenye kampeni yake kuibana Russia, kwa kuitaka ishiriki kwenye vikwazo na kukatisha biashara na Russia. Bahati mbaya ni kuwa China haina sababu ya kufanya hivyo, kwa hiyo masikitiko ya Marekani kushindwa kuilazimisha China itii nia yake, kunaifanya ianze kuipaka matope China.

Lengo la pili ni Marekani kutafuta uungaji mkono wake kwenye mkakati wake wa Indo-Pasifiki ambao ajenda yake kuu ni kuizingira China. Marekani imekuwa ikiendelea na mpango wake wa muda mrefu wa kuizingira China kwa visingizio mbalimbali, lakini nchi za Ulaya zinazotambua haki na zinazosisitiza kuwa na sera huru ya mambo ya nje, haziungi mkono sera hiyo ya Marekani. Jaribio la kuitaja China kuwa ni “msaidizi wa Russia” lengo lake ni kutaka kupata uungaji mkono wa nchi za Ulaya kwenye kutekeleza huo mkakati wake. Hata hivyo njia hiyo pia inaonekana kugonga mwamba.

Tayari nchi mbalimbali duniani zimeonyesha misimamo kuhusu mgogoro wa Ukraine. Kuna zile zinazoiunga mkono Russia, kuna zinazopinga, na kuna zisizopendelea upande wowote, maamuzi hayo yote yanatakiwa kuheshimiwa. Demokrasia kwenye utaratibu wa kimataifa inatoa uhuru kwa nchi zote kufanya maamuzi yake kwa mujibu wa mazingira na mahitaji yake. Kitendo cha Marekani kutaka nchi nyingine ziiunge mkono kwa nguvu, au kuzipaka matope nchi zinazokataa kufuata inachotaka, ni kupuuza demokrasia kwenye siasa za kimataifa na kuendekeza umwamba. Kamwe matokeo yake hayatakuwa mazuri.
 
Alafu unalalamika kupanda bei mafuta.
 
Unahangaika bure tuu huyo Puttin ni kichaaa, na anatakiwa awe mirembe haraka sana... Leo hii mafuta yamefikia 3400 huku Kigoma na before long itafika 4000 Sasa wewe endelea kujifanya ndezi halafu utajua hujui...
 
View attachment 2213312

Andiko bora kabisa
 
Pamoja na yote hayo pia Marekani ananufaika sana na hiyo vita ya Ukraine kwa kuuza mafuta kwa kiwango kikubwa huko EU.
Pia silaha anazopenyeza huko zinawekwa kwenye kumbukumbu...mwisho wa siku atalipwa.

Marekani wanafiki sana.
 
Unahangaika bure tuu huyo Puttin ni kichaaa, na anatakiwa awe mirembe haraka sana... Leo hii mafuta yamefikia 3400 huku Kigoma na before long itafika 4000 Sasa wewe endelea kujifanya ndezi halafu utajua hujui...
si utumie ya mawese shemeji shida nini!?
 
Kitendo cha Marekani kutaka nchi nyingine ziiunge mkono kwa nguvu, au kuzipaka matope nchi zinazokataa kufuata inachotaka, ni kupuuza demokrasia kwenye siasa za kimataifa na kuendekeza umwamba. Kamwe matokeo yake hayatakuwa mazuri.

Kitendo cha Urusi kuvamia Taifa huru ili kulishinikiza lisifanye maamuzi wanayoona yana manufaa kwao ndiyo kuheshimu Demokrasia Mkuu?
 
Bado sijaona kosa kwa Marekani.anacho jaribu ni kumshikiza Putin kuondoa jeshi lake Ukraini basi.
 
View attachment 2213312

Fadhili Mpunji

Mgogoro wa Ukraine unaendelea kufichua hali ya umwamba kwenye siasa za kimataifa, ambao sasa umefikia hatua ya nchi moja kuzilazimisha nchi nyingine kufuata msimamo wake, na kufanya vitendo vya kulenga nchi zisizokubaliana na hali hiyo. Kwa baadhi ya nchi za magharibi, dhana kuhusu uhuru wa nchi kufanya maamuzi kwa mujibu wa maslahi yake na mazingira yake, ambayo ni msingi wa uhusiano wa kimataifa inawezekana tu na inaheshimiwa pale maamuzi hayo yanapokuwa na manufaa kwa nchi za magharibi. Vinginevyo dhana hiyo ni maneno matupu.

Hivi karibuni Marekani na washirika wake wamekuwa wakitumia njia mbalimbali za kutoa shinikizo kupinga operesheni ya Russia nchini Ukraine, ikiwa ni pamoja na kutoka nje kwenye mkutano wa kundi la G20 kuonyesha kuisusia Russia, na kuweka msururu wa vikwazo fedha ili kudhoofisha uwezo wa Russia kuendesha operesheni yake. Licha ya kuwa jambo hili si la kufurahisha, lakini wachambuzi wa maswala ya kisiasa wanaona ni moja ya njia zinazotumika kwenye migogoro. Lakini kinacholeta ukakasi ni pale ambapo Marekani na washirika wake wanajaribu kuzilazimisha nchi nyingine zifuate msimamo wao, au kuzitaka ziitii na kuchukua hatua kama inavyotaka Marekani, bila kujali maoni ya nchi hizo kuhusu mgogoro wenyewe.

Mara nyingi China imekuwa ikirudia mara kwa mara msimamo wake wa siku nyingi wa kutopendelea upande wowote kwenye migogoro, na kuhimiza njia ya mazungumzo kuwa ufumbuzi sahihi wa mgogoro huo. Nchi kadhaa ikiwa ni pamoja na nchi za Afrika, pia zimeonesha msimamo kama huo kwenye mgogoro wa Ukraine. Lakini Marekani imeanza kuipaka matope China kwa kuendelea na urafiki wa muda mrefu na Russia katika kipindi hiki ambapo kuna mgogoro na Ukraine, kwani inahisi au inahofu kuwa urafiki huu unaweza kuikwamisha kwenye malengo yake. Kwa hiyo inailazimisha China kuipinga Russia, na pale China inapokataa kufanya hivyo au inapokuwa kimya, inaitaja China kuwa ni “msaidizi wa Russia”. Wachambuzi wa maswala ya kimataifa wanaona hali hii si ya ajabu, bali ni janja ya siku zote ya Marekani yenye malengo mawili.

Lengo la kwanza ni kutaka nchi za Ulaya ambazo ni washirika wa Marekani ziichukie China. Ukweli ni kwamba vikwazo vilivyowekwa na Marekani na nchi za magharibi dhidi ya Russia, licha ya kuathiri uchumi wa Russia pia vimekuwa ni mwiba mchungu kwa nchi za Ulaya ambazo zimeanza kushuhudia kupanda kwa gharama za maisha. Inachofanya Marekani ni kutaka nchi za Ulaya zione kuwa uchungu huo unaotokana na kukatishwa kwa biashara ya mafuta na gesi na Russia, unatokana na baadhi ya nchi kutoipinga Russia, na haukusababishwa na Marekani. Kwa hiyo inachofanya Marekani ni kuzusha “maadui wa kufikirika” kuwa ndio chanzo cha taabu za watu wa Ulaya, na kujaribu kuwaaminisha watu wa Ulaya kuwa sio vikwazo vilivyowekwa na Marekani na washirika wake, bali ni China na Russia ndio sababu ya taabu zao.

Profesa Diao Daming wa Chuo Kikuu cha Renmin cha Beijing, amesema toka mwanzo Marekani ilikuwa inaweka mazingira ya kuishinikiza China ijiunge kwenye kampeni yake kuibana Russia, kwa kuitaka ishiriki kwenye vikwazo na kukatisha biashara na Russia. Bahati mbaya ni kuwa China haina sababu ya kufanya hivyo, kwa hiyo masikitiko ya Marekani kushindwa kuilazimisha China itii nia yake, kunaifanya ianze kuipaka matope China.

Lengo la pili ni Marekani kutafuta uungaji mkono wake kwenye mkakati wake wa Indo-Pasifiki ambao ajenda yake kuu ni kuizingira China. Marekani imekuwa ikiendelea na mpango wake wa muda mrefu wa kuizingira China kwa visingizio mbalimbali, lakini nchi za Ulaya zinazotambua haki na zinazosisitiza kuwa na sera huru ya mambo ya nje, haziungi mkono sera hiyo ya Marekani. Jaribio la kuitaja China kuwa ni “msaidizi wa Russia” lengo lake ni kutaka kupata uungaji mkono wa nchi za Ulaya kwenye kutekeleza huo mkakati wake. Hata hivyo njia hiyo pia inaonekana kugonga mwamba.

Tayari nchi mbalimbali duniani zimeonyesha misimamo kuhusu mgogoro wa Ukraine. Kuna zile zinazoiunga mkono Russia, kuna zinazopinga, na kuna zisizopendelea upande wowote, maamuzi hayo yote yanatakiwa kuheshimiwa. Demokrasia kwenye utaratibu wa kimataifa inatoa uhuru kwa nchi zote kufanya maamuzi yake kwa mujibu wa mazingira na mahitaji yake. Kitendo cha Marekani kutaka nchi nyingine ziiunge mkono kwa nguvu, au kuzipaka matope nchi zinazokataa kufuata inachotaka, ni kupuuza demokrasia kwenye siasa za kimataifa na kuendekeza umwamba. Kamwe matokeo yake hayatakuwa mazuri.
Kaa nchi kawatu kalinyang'anywa eneo kalituli bado haitoshi wanataka Nchi nzima Slava Ukrain.
 
Hakuna Rais mjinga kama VP wa Russia yani kajiua kuvamia Ukraine !!! Huu ndio mwanzo wa mwisho wako!!!USA ilikuwa inamtafuta kitambo sasa imempata vilivyo!!!Ila Watanzania hawaelewii
 
Back
Top Bottom