Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Waziri wa ulinzi wa Marekani Mark Esper amekanusha madai kuwa majeshi yake yanataka kuondoka Iraq, baada ya barua kutoka kwa jenerali wa Marekani kupendekeza waondoke.
Barua ilisema kuwa Marekani itaondoa vikosi vya majeshi yake siku zijazo au wiki baada ya wabunge wa Iraq kuwataka waondoke.
Bwana Esper alisema kuwa hakuna maamuzi yeyote ya kuondoka ambayo yaliondolewa.
Mkanganyiko huu wa vitisho ulikuja mara baada ya jeshi la Marekani kumuua kamanda wa jeshi wa Iran Qasem Soleimani.
Jenerali Soleimani aliuawa katika mapambano ya anga huko Baghdad siku ya ijumaa baada ya rais Trump kuamuru wafanye hivyo.
Inaonekana kuwa barua iliyotumwa na Brigedia Jenerali William H Seely, Mkuu wa jeshi la Marekani katika kikosi kilichopo Iraq, kwenda kwa mkurugenzi msaidizi wa opereshani ya pamoja Abdul Amir,
Barua ilianza hivi: "Ndugu, kwa heshima ya Jamuhuri ya Iraq, na maombi yaliyotolewa na bunge la Iraq, pamoja na waziri mkuu na mkuu wa operesheni za pamoja (Combined Joint Task Force) tutaondoa vikosi vyetu vya jeshi katika siku zijazo au wiki kadhaa ili kujiandaa na hatua nyingine .
Barua ilisema kuwa hatua kadhaa zitafanyika ikiwa pamoja na kuwa na ndege nyingi angani wakati wa saa za usiku ili kuhakikisha kuwa wanaondoka kwa usalama na utaratibu unaofaa.
Vilevile hatua hii itaondoa mitazamo kuwa labda tuna mpango wa kuongeza majeshi zaidi katika ardhi ya Baghdad.
Bwana Esper aliwaambia waandishi wa habari nchini Marekani: "Hakuna hatua yeyote iliyofanywa kuhusu majeshi ya Marekani kuondoka Iraq. Sifahamu chochote kuhusu barua hiyo... Tunajaribu kufuatilia kujua barua hiyo imetokea wapi na ina maana gani?
"Kiufupi, hatujafanya maamuzi ya kuondoka Iraq."
Kiongozi wa juu wa jeshi la Marekani, Mark Milley, alisema pia kuwa barua hiyo ilikuwa ya kimakosa.
Kwa sababu ilikuwa imeandikwa vibaya, haikuwekwa sahihi na haikupaswa kutolewa. Ilikuwa ikisambazwa kwa ajili ya kuongeza maelezo, kutoka kwa Wairaqi pia.
"Barua ilitumwa kwa baadhi ya viongozi wa jeshi la Iraq ili kuweka utaratibu wa usafiri wa anga pamoja na mambo mengine muhimu. Na barua ilitumwa kwao na kuanza kusambazwa kwa watu na sasa imeleta mtazamo wa uhasama."
Jenerali Milley alirudia pia kusema kuwa jushi la Marekani haliondoki Iraq.
CHANZO: BBC