Watanzania
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 727
- 44
Date::3/19/2010: Mwananchi
Marekani yashupalia vita dhidi ya rushwa
Na Boniface Meena
SERIKALI bado inalegalega katika mapambano dhidi ya rushwa hali ambayo imechagia baadhi ya viongozi wa serikali kujuhusisha na rushwa pamoja na wizi wa fedha za umma, ripoti ya haki za binaadamu ya mwaka 2009 imeeleza.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa hivi karibuni na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, serikali imekuwa haisimamii sheria na hivyo kusababisha viongozi wa ngazi za juu serikalini kuchukua rushwa na kufanya matumizi mabaya ya fedha za serikali wakati wakijua ni kinyume cha sheria.
Ripoti hiyo imegawanywa katika vipengele vikuu saba ambavyo ni heshima kwa utu wa mtu; heshima kwa haki za msingi; heshima kwa haki za kisiasa; rushwa na uwazi kwa serikali; mwelekeo wa serikali kwa kuzingatia ukiukwaji wa haki za binadamu, ubaguzi, ukatili wa kijamii na usafirishaji wa binadamu na kipengele cha mwisho ni haki za wafanyakazi.
Imeeleza kuwa Benki ya Dunia (WB) ilieleza kuwa rushwa imekuwa ni tatizo kubwa na vyombo vya habari vikaitaka serikali kupambana vikali na tatizo hilo kwani kutokufanya hivyo kunafanya wizi wa fedha za serikali na rushwa kuendelea.
Pia imeeleza kuwa pamoja na kwamba baadhi ya viongozi wameshtakiwa kwa kujihusisha na rushwa pamoja na matumizi mabaya ya fedha za serikali, kesi hizo zimekuwa zikiendeshwa taratibu kitu ambacho hakileti matumaini.
Pia ripoti hiyo imeeleza jinsi gani rushwa ilivyoichafua sekta ya mahakama kutokana na baadhi ya mahakimu kushtakiwa na kufungwa kwa makosa ya kuomba rushwa ili wapindishe sheria.
Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (Takukuru) ndiyo inaohusika na kutoa elimu kuhusu rushwa, kuchunguza na kushtaki watuhumiwa kwa kushirikiana na DPP.
Lakini ripoti hiyo inaeleza kuwa pamoja na hayo kumekuwa na maendeleo finyu kwani imeeleza kuwa asilimia 20 ya bajeti ya serikali kila mwaka imekuwa ikipotelea kwenye rushwa.
Hiyo ikiwa ni pamoja na wizi, matumizi mabaya ya fedha za serikali, manunuzi na mishahara kwa wafanyakazi hewa.
Pia imeeleza kushangazwa na mawaziri ambao wanateuliwa kutotaka kutangaza mali zao na kufanya suala hilo kuwa la usiri mkubwa.
Kutokuwa na sheria ambayo inaruhusu kupata taarifa za serikali kumefanya upatikanaji wa taarifa muhimu kuwa tatizo kubwa kwa kuwa wafanyakazi wa serikali wamekuwa wagumu kutoa taarifa kitu ambacho ni kibaya.
Ripoti hiyo imetaja vipengele saba vya sheria ambavyo vimekuwa havifuatwi wala kusimamiwa kwa umakini na kusababishwa zikiukwe.