Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Wizara ya ulinzi ya Marekani imesitisha kwa kiasi fulani mafunzo ya marubani wa kijeshi kutoka Saudi Arabia kufuatia lile shambulizi katika kambi ya kijeshi ya Marekani mjini Florida.
Kulingana na wizara hiyo wanajeshi hao zaidi ya mia tatu hawatapokea mafunzo yoyote hadi taarifa zaidi itakapotolewa. Lakini mafunzo ya darasani kama kufunzwa Kiingereza yanatarajiwa kuendelea kutolewa.
Siku ya Ijumaa mwanajeshi mmoja wa Saudi Arabia alifyatua risasi katika kambi ya kijeshi ya Pensacola huko Florida na kuwauwa watu watatu. Wachunguzi wanasema huenda ikawa shambulio hilo lilichochewa na masuala ya ugaidi.
Kufikia sasa hakuna ishara yoyote ya mwanajeshi huyo kushirikiana na mtu yeyote katika kufanya shambulizi hilo.