Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Katika juhudi za kupamba na mripuko wa #CoronaVirus rais wa Marekani Donald Trump amepiga marufuku wasafiri kutoka Brazil
Afisa habari wa Ikulu ya Kayleigh McEnany amesema kuanzia Mei 28, watu wote wasio raia wa Marekani ambao wamekuwa nchini Brazil katika muda wa siku 14 zilizopita, hawataruhusiwa kuingia nchini Marekani, na kuongeza kuwa hatua hiyo ni juhudi ya kuepusha maambukizi mapya kutoka nje ya nchi
Marufuku hiyo haitawahusu raia wa Marekani wanaorejea nyumbani, na pia wale wenye vibali vya kudumu vya kuishi nchini humo.
Bolsonaro aendelea kutojali Brazil ambayo hivi sasa inavyo visa vipatavyo 367,000 vya corona na imerikodi vifo zaidi ya 22,000 kutokana na virusi hivyo, ipo katika nafasi ya pili kuwa na idadi kubwa ya maambukizi ya COVID-19, ikitanguliwa tu na Marekani.
Licha ya hali hiyo, Rais wa Brazil Jair Bolsonaro anaendelea kuubeza mripuko wa janga hilo la corona, akishikilia kuwa ni mafua ya kawaida. Wizara ya mambo ya nje ya Brazil imesema haikuipa umuhimu mkubwa marufuku hiyo ya safari ya Marekani, ikiitaja kuwa ni mchakato wa kawaida wa tahadhari.
Source: Dw