Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Serikali ya Marekani imetenga dau la $25M kwa yeyote atakayesaidia au kufanikisha kukamatwa kwa Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro kwa makosa ya ugaidi wa dawa za kulevya(Narco- terrorism).
Serikali ya Marekani inamtuhumu Maduro na viongozi kadhaa waandamizi wa Venezuela kufanikisha, kuchochea na kutumia biashara ya madawa ya kulevya ya Cocaine kama silaha ya kudhuru raia wa Marekani. Mwaka 2020 serikali ya Trump ilitenga kwa mara ya kwanza dau la $15M kukamatwa kwake na mwaka huu serikali ya Biden imeongeza dau hilo kufikia $25M.