Marekebisho ya sheria ya hifadhi za mfuko wa jamii yamekiuka haki za binadamu

Marekebisho ya sheria ya hifadhi za mfuko wa jamii yamekiuka haki za binadamu

Indume

Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
81
Reaction score
37
Ndugu wana JF,Nimesoma na kufuatilia kwa makini Marekebisho ya Sheria yaHifadhi za jamii na nimegundua kuna masuala ya msingi ambayo hayakuzingatiwa.Ukiangalia Katiba ya nchi ibara ya 21, inatakiwa mwananchi ashirikishwe katikamaamuzi mbalimbali lakini katika hili la mifuko ya jamii ushirikishwajihaukuwepo, na kama ulikuwepo basi ulikuwa kidogo sana.
Ukiangalia kile kinachosemwa katika marekebisho ya sheriahii kuwa mwanachama atakuwa na haki ya kukopeshwa nyumba. Hebu fikiria kima chachini cha mtanzania wa leo, atachangia shilingi ngapi ili iwe collateral naakopeshwe nyumba?? Unadhani kama ndo anaanza kazi akiwa na miaka 35 na ana kimacha chini unadhani atakopeshwa hiyo nyumba atakapokuwa na miaka baada ya 55wakati huenda hiyo nyumba itakuwa na thamaniya shilingi million 50?? Na kwa nini mtu alazimishwe kukopa nyumba?? Kuna sirigani hapo?? Kwa nini wasiongelee labda bishara zingine tofauti na nyumba??
Life expectancy ya Mtanzania ni miaka 45. Ina maana kuwawachangiaji wa mifuko ya kijamii huenda wasifaidike na michango yao maanawengine watakuwa wametangulia mbele ya haki. Kwa hali hii inaonekana kuwasheria hii inalenga michango yetu iwe madai ya mirathi. Na kama lengo nikumsaidia mchangiaji basin i vema akapata mafao yake mara tu anapoacha kazi,kufukuzwa ama mkataba kuisha illi aweze kujishughulisha na shughuli zingine kwaufanisi zaidi akiwa na nguvu chini ya miaka 55.
Hebu tumuangalie huyu mchangiaji ambaye leo ana miaka kama30 au 40 anaacha kazi au mkataba unaisha na anaamua kwenda shule kozi yoyote kujiendeleza kielimu. Kwa marekebisho haya yasheria itambidi asiende shule asubiri awe na miaka zaidi ya 55 ndoakajiendeleze kielimu. Unadhani kwa kipindi hicho ambacho atakuwa amekaaanasubiri kufikisha miaka 55 unadhani akili yake itakuwa bado inawaza kwendashule? Hapo ni lazima juhudi zifanyike ili kumwezesha mchangiaji huku awezekwenda shule akiwa na nguvu mapema. Maana kwa hali halisi ya Tanzania akiwa namiaka 55 kama ataamua kuchukua digree atakuwa na miaka 58, akiongeza na mastersatakuwa na zaidi ya miaka 60. Je wapi ataajiriwa tena wakati kila sikumatangazo ya kazi toka serikalini huwa wanasema mwombaji wa kazi asizidi miaka35??
Pesa yetu inashuka thamani kila siku. Je marekebisho hayahayakuzingatia pale baada ya miaka 55 kama kutakuwa na ongezeko la pesakulingana na kushuka kwa thamani ya shilingi yetu.
Mwisho hebu tuwaangalie wachangiaji ambao kwa namna Fulani niwagonjwa kiafya (mfano Ukimwi) auwategemezi wao ni wagonjwa na wanategemea mafao hayo yawasaidie kwa matibabu.Kwa marekebisho ya sheria hii itawabidi wasubirie hadi wafikishe miaka 55 ndowaende hospitalini kwa matibabu. Kwa hali halisi watakuwa huenda wamekufa.Ndugu zangu kwa mtazamo wangu naona haki za binadamu (Haki ya kuishi)haikuangaliwa hapa. Pia serikali hii iliyopo madarakani haina record ya kulipamafao. Ebu jikumbushe na rejea jinsi wazee wastaafu wa lililokuwa shirikisho laAfrica Mashariki. Toka mwaka 1977 wengine hawajalipwa! Itakuwa wewe wa 2012,itakuchukua hadi 2097!
Serikali imepewa dhamana ya kutunza michango ya wanachama wamifuko ya jamii tu. Ni vema wachangiaji washirikishwe kila inapohitajika kuwepokwa marekebisho mbalimbali nan i vema mchangiaji ndiye aamue muda wa kuichukuana namna ya kuitumia kwa kuzingatia maisha halisi ya mtanzania wa leo. Naomba marekebisho ya sheria ya hifadhi zajamii yasianze kutumika ili wachangiaji ndio watoe namna ya kuendesha mafaoyao/michango yao.
Nawasilisha na nipo tayari kukosolewa!!
 
KuNa haja ya kufuatilia zile hansard wakati wanapitisha hii sheria
Maana haingii akilini waliipitishaje hii bungeni
 
Wateule wachache walio-qualify katika "mradi" huu ni pamoja na Rais...ndio maana alisaini haraka akijua yeye ametangulia umri...Pili tuna Rais ambaye hana haja ya kujali maslahi ya watu anaowaongoza,!! Akifika mbele ya haki "Atawajibika kujibu maswali mengi ambayo ki ukweli, sidhani kama atakuwa na majibu". Hivyo basi itabidi malaika wa zamu wamuwajibishe.
 
Kuanzia ssra,rais aliyesain na wabunge waliopitisha huu utumbo sidhani kama walivaa viatu vya wafanyakazi na kwakujua hilo ssra wakawarubuni wabunge kwamba wao haiwahusu ndio maana wakaunga hoja mojakwamoja,pili ssra watambue kuzuia fao la kujitoa linapingwa sio tu na wana migodi hata sector nyingine tunapinga huo ungese!!
 
Back
Top Bottom