Maria Sarungi ni mwanaharakati kutokea Tanzania, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu, utawala wa kisheria unaozingatia misingi ya kidemokrasia. Maria amekuwa akijihusisha na masuala mbalimbali ya siasa kwa kipindi kirefu sasa, amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kuendsha harakati zake ikiwemo X zamani ikijulikana kama twitter ambapo amejizolea umaarufu mkubwa.
Katika
uchaguzi mkuu uliofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA, Maria alikuwa ni moja kati ya wafuatilizi wa uchaguzi huo huku akisisitiza uhitaji wa mabadiliko ndani ya chama hicho. Mara baada uchaguzi kukamilika Tundu Lissu akimshinda Freeman Mbowe aliyekuwa akitetea kiti hicho kupitia ukurasa wake wa X, Maria
alikipongeza chama hicho kwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa na kutoa mfano bora kwamba siasa zinaweza kufanyika kwa uwazi.
Kumekuwapo na Chapisho linalosambaa mtandaoni likiwa na taarifa inayosema Maria Sarungi aitabiria kifo CHADEMA.
Je ni upi uhalisia wa chapisho hilo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa Kurasa za mitandao ya kijamii za Maria Sarungi
hazikuchapisha madai hayo yanayofafanuliwa kama utabiri wa kifo cha CHADEMA.
Aidha mnamo tarehe 21, Januari 2025
Millard Ayo hakuchapisha taarifa hiyo katika kurasa zake za mitandao ya kijamii bali chapisho hilo lilitumia utambulisho wa Millard Ayo ili kuuaminisha umma kuwa ni taarifa ya kweli.
Si mara ya kwanza juu ya uwepo wa taarifa za upotoshaji zikihusisha CHADEMA na mwanaharakati huyo. Tazama
hapa.