🛑 TAARIFA YA KUSIKITISHA
Mwenyekiti wa Chadema (T) ndg. Tundu Lissu amepata ajali mbaya akiwa njiani kuelekea mkoani Singida kushiriki mazishi ya kaka yake..taarifa rasmi ya vifo na majerui nitawajuza lakini hali zao ni mbaya sana wamevuja damu nyingi mnaombwa mfike hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa kujitolea Damu kwa waliopo Dodoma.
Mwenyekiti wa Chadema (T) ndg. Tundu Lissu amepata ajali mbaya akiwa njiani kuelekea mkoani Singida kushiriki mazishi ya kaka yake..taarifa rasmi ya vifo na majerui nitawajuza lakini hali zao ni mbaya sana wamevuja damu nyingi mnaombwa mfike hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa kujitolea Damu kwa waliopo Dodoma.
- Tunachokijua
- Tundu Lissu ni mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye alichaguliwa kutumikia nafasi hiyo mnamo Januari 21, 2025.
Madai
Kumekuzuka ujumbe kwenye mitandao ya kijami ikidaiwa kutolewa na Maria Sarungi Tsehai kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu amepata ajali alipokuwa akielekea kwenye mazishi ya kaka yake.
Uhalisia wa taarifa hiyo
JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo na kubaini kuwa si ya kweli na Taarifa hiyo haipo katika ukurasa rasmi wa Maria Sarungi.
Ufuatiliaji wa kimtandao kupitia Google reverse image search tumebaini kuwa picha zilizotumika katika taarifa hiyo si za hivi karibuni bali na za tukio la ajali iliyotokea Septemba 21, 2021 ambapo aliyekuwa mkurugenzi wa Dar Mpya John Marwa hivi sasa akiwa na Jambo Tv alikuwa ni miongoni mwa waliopata ajali hiyo, wengine ni mwandishi wa Global Tv Mohamed Zengwa na mwenzao mmoja wakiwa na gari aina ya Land Cruiser T 835 DRR, Mkoani Tabora. Tazama hapa na hapa.
Kwenye ukurasa rasmi wa X wa CHADEMA wameandika kuwa;
"Lissu ataongoza viongozi na wanachama katika mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti wa Chama Mkoa wa Manyara na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kanda ya Kaskazini ndugu Derick Magoma, tarehe 11 Februari 2025 kijijini kwao Matufa, Mji wa Magugu, wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara".
Aidha hakuna taarifa yoyote iliyotolewa hivi kribuni kuhusu kifo cha anayedaiwa kuwa ni kaka yake Lissu.