Mariah Carey aipiga bei pete yake ya ndoa...Apata mamilioni

Drone Camera

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2017
Posts
14,041
Reaction score
13,907
Sio Bongo tu ambapo wanawake hujiongeza kwa kuuza pete za uchumba pale mambo yanapokwenda kombo.

Mwanamuziki tajiri duniani, Mariah Carey ‘ameipiga bei’ pete ya uchumba aliyovalishwa na mchumba wake wa zamani, bilionea James Packer kwa Dola 2.1 milioni za Marekani ikiwa ni bei ya ‘kutupa’.

Msemaji wa mwanamuziki huyo amesema ameamua kuiuza ili aendelee na maisha kwa kuwa hataki kubaki na kitu kinachomkumbusha mambo yaliyopita.

Inaelezwa kuwa Packer aliinunua pete hiyo kwa Dola 10 milioni za Marekani ambazo ni zaidi ya Sh2.2 bilioni.

source: Mwananchi
 
$2.1M ni bei ya kutupa sana.
 
Kutoka Dolla Million 10 Mpka Dola Million 2....Gap Kubwa Sanaaa!! Mangi HaweziFanya Hii Biashara Mama Angu Aisee!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…