Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 80
Niliwahi kuandika siku za nyuma mkakati mzima wa Rostam na ule wa Gachuma. Na katika kuandika nikamtaja na mtu mmoja aliyeitwa Mariam Chacha Wangwe. Niliacha kuendelea kuandika kwa heshima ya marehemu. Sasa mke wa marehemu amepanga kuendelea na ile mikakati niliyoieleza wakati ule. Ameanza kwa kujitokeza hadharani kusema kwamba anataka Spika wa Bunge aunde Tume ya kuchunguza kifo cha Wangwe. Amewajia juu CHADEMA kuwa wamekwepa kumzika marehemu mumewe na ameonyesha kuwa viongozi wa CHADEMA wanahusika na utata wa kifo hicho.
Hata hivyo, mkakati mzima umepata upinzani ndani ya familia kwa kuwa mke mkubwa wa marehemu anamlaumu Mariam kuwa ni kimada aliyepora mume na mali zote za marehemu. Kwa sasa sinafanywa jitihada za hali ya juu na Gachuma kuwaweka sawa watoto wakubwa wa marehemu ambao wameanza kubaini Mariam anawatumia kwa minajili ya kuchota fedha wakati wao hawapi mgao wowote.
Kwa upande mwingine, bwana Mengi amepata shinikizo toka kwa wamiliki wengine wa vyombo vya habari kupitia MOAT kuwa ahakikishe ripoti ya Jukwaa la Wahariri haitoki kabla ya uchaguzi Tarime kufanyika. Na Mwenyekiti wa jukwaa hilo Sakina Datoo naye ametishiwa kuwa akitoa ripoti hiyo tu, vyombo hivyo vya habari vitamtangaza kuwa anafanya kazi ya kuunga mkono CHADEMA ili ishinde uchaguzi tarime.
Katika mazingira hayo, inaelekea ripoti hiyo yenye kueleza kama kulikuwa na mapanga au la na inayoeleza ukweli au uwongo kuhusu kupikwa kwa habari sasa itapaswa iwekwe kabatini. Kamba yangu ya kupata habari imekatika baada ya Ballile kuondolewa kuwa mhariri wa Rai. Sasa hajadiliani tena na wenzake na hivyo chanzo changu cha habari kimekwama kupata habari za upande wa pili. Na toka uzinduzi mpya wa magazeti yetu ufanyike mimi na wenzangu watatu wametuhamishia The African ambapo kwa kweli hakuna nyeti za maana.
PM