Maridhiano kwetu yanakosa chachandu ya rungu la umma

Maridhiano kwetu yanakosa chachandu ya rungu la umma

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kwa mara nyingine elimu haina mwisho na ni mburula pekee mwenye kuamini kuwa kafika.

Hapo kwa majirani Ruto na Kenya Kwanza wanapelekwa mpera mpera. Kisa na mkasa kitisho cha uhakika cha nguvu ya umma kilichopo kama maridhiano yatakwama.

Kwamba:

IMG_20230531_051325.jpg

Tayari mambuzi wa huko wako kwenye vidole gumba (on their toes):

Screenshot_20230531-050953.jpg

Raila meets MPs as Kenya Kwanza now moves to save talks

Maridhiano hayawezi kuwa kwa mapenzi au utashi wa mtu au chama.

Nchi ni ya wananchi!
 
Mbowe ni mtu wa Serikali hawezi kukataa Uteuzi wowote hata akiteuliwa kuwa DC atahudumu!

Usichanganye Mbowe na kina Lijualipole waliojunasibu hadharani kufanya kazi yoyote wakiteuliwa.
 
Nakwambia Mbowe alikataa biashara ya uwaziri chini ya jiwe!

Wangapi waliupewa?

Hizi ni habari mpya kwako?
Ni kwa sababu Wewe umemjulia Mbowe hapo Ufipa ndio unaaminishwa hizo hadithi za Chekechea!
 
Kama raia wakijitambua, hata viongozi wanaowaongoza hupata nguvu ya kuendeleza harakati ili kufikia malengo, wakijua kuna uungwaji mkono nyuma yao, hicho ndicho kinachomkuta Odinga pale Kenya mpaka kumfanya Ruto aione hali ilivyo chungu.

Hapa kwetu hali ni tofauti, na ni kinyume kabisa na kinachotokea Kenya, raia wamelala, baadhi ya viongozi ndio wameamka, huku wengine wakitumiwa na mtawala kwa mapenzi yao, sisi bado tuko disorganised kwa kiwango kikubwa sana.
 
Ni kwa sababu Wewe umemjulia Mbowe hapo Ufipa ndio unaaminishwa hizo hadithi za Chekechea!

Waonyesha kuwa makasiriko sana na Mbowe, kuliko hata jiwe. Kulikoni ndugu, alikupokonya kitu?
 
Waonyesha kuwa makasiriko sana na Mbowe, kuliko hata jiwe. Kulikoni ndugu, alikupokonya kitu?
Unapewa tu Maarifa bwashee

Usijidanganye Eti Chadema Chini ya Freeman watafanya zaidi ya hiyo ya kupigiwa salute

Akina Wamalwa ni mabepari wale siyo Watu wa Mishahara kama Viongozi wa Chadema
 
Kama raia wakijitambua hata viongozi wanaowaongoza hupata nguvu ya kuendeleza harakati ili kufikia malengo, hicho ndicho kinachomkuta Odinga pale Kenya mpaka kumfanya Ruto aione hali ilivyo chungu.

Hapa kwetu hali ni tofauti, na ni kinyume kabisa na kinachotokea Kenya, raia wamelala, baadhi ya viongozi ndio wameamka, huku wengine wakitumiwa na mtawala kwa mapenzi yao, sisi bado tuko disorganised kwa kiwango kikubwa sana.

Hii itakuwa kutowatendea haki wananchi wakiwamo waliopoteza maisha yao, kujeruhiwa, kufungwa nk, kwenye kuipagania haki nchini hapa.

Hapa chini ni watanzania:

Uthibitisho upi zaidi unataka?

Mifano iko mingi ila Cha msingi:

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

Viongozi rojo rojo wangepumzika kupisha damu inayochemka kama bahari. SI lazima tufikie kwenye kufurushana.

Tuna matatizo ya kiuongozi zaidi.
 
Hii itakuwa kutowatendea haki wananchi wakiwamo waliopoteza maisha yao, kujeruhiwa, kufungwa nk, kwenye kuipagania haki nchini hapa.

Hapa chini ni watanzania:

View attachment 2640888

Uthibitisho upi zaidi unataka?

Mifano iko mingi ila Cha msingi:

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

Viongozi rojo rojo wangepumzika kupisha damu inayochemka kama bahari. SI lazima tufikie kwenye kufurushana.

Tuna matatizo ya kiuongozi zaidi.
Hawa wananchi wanaoburuzwa kila siku halafu wanasubiri mpaka waje kuamshwa na viongozi kukumbushwa maumivu wanayopitia, ni wajinga tu, hawajielewi, na hawa wanajichelewesha, wala hawacheleweshwi na hao viongozi "rojo rojo" kama unavyodai wewe.

Tazama wale wakenya kule kwao, hata kama Odinga akilala nyumbani, wao wataamka waendelee na harakati zao, vipi sisi, kwanini kila siku tunasubiri mpaka tuamshwe? are we robots?! tozo, upandaji wa gharama za maisha kila siku, tumelala tu!.

Mjomba ukumbuke tu msemo wa waswahili; unaweza kumpeleka n'gombe kunywa maji, lakini huwezi kumlazimisha ayanywe!, viongozi wetu wamechoka.
 
Kuna asali zaidi wanalamba kuliko mawaziri?

Hukuwahi kumsikia Mwamba aliahidiwa uwaziri na jiwe na bado akaupiga chini?
Story za vijiweni hizo. Endeleeni kumsindikiza Mbowe anabugia tu asali!!!

Mpinzani wa kweli hapo ni Lisu tu
 
Back
Top Bottom