USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 10,904
- 26,184
Chadema wana furaha, wanatabasamu usoni mwao, je nini wanafurahia!? kula asali ni kuongea maneno ya busara, sasa Chadema wanaongea mambo ya busara na kutenda kwa busara, je wanakosea? amani ndio msingi.
Je, Chadema wameacha harakati zao kutaka kushika dola, ndio hawana dhamira ya kushika dola kupitia uchaguzi ujao wa mwaka 2025,sasa nini dhumuni lao, je ni mtego kwa Chadema? Hapana, je ni mtego kwa CCM? Hapana, Chadema imeacha kushughulika na shida za Wananchi? hapana, je Chadema imedhamiria kuacha yote na kuitafuta katiba mpya? labda ndio kipaumbele chao.
Kama unajua wanachofikiri Chadema hebu nikuulize maswali haya:
1. Hivi Chadema wanafanya siasa za namna gani eti?
2. Kama Chadema wanaona mambo ni shwari, je ni kwa namna gani siasa zao "hazilitakii mema au zinalitakia mema taifa hili zuri la Tanzania? Je unadhani Upinzani umekufa hapa Tanzania na kinachofanyika sasa ni kuzika tu, ni dhahiri Chadema wameondoka kwenye misingi iliyowainua kupitia harakati zao za kutetea Wananchi mfano "operation sangara" iliyoendeshwa vyema na Daktari Wilbrod Slaa mwaka 2009 na kuzalisha mafuriko katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Sasa Chadema wanatenda kama vile wapo kwenye Coalition Government au Serikali ya Umoja wa kitaifa(SUK) au GNU (Government of National Unity) ambayo tumewahi kuiona uko Tanzania Visiwani Zanzibar, Mtu au kikundi chochote kikiondoka kwenye misingi, matokeo yake ni kufa au kuzaliwa kwa namna nyingine ya kikundi au chama,inaweza kuwa kama (chemical change) kwenye kemia,yaani chama kinakuwa tofauti kabisa na kile chama cha awali.
Lengo la chama cha siasa ni kushika madaraka na dola ya nchi kutumika kwa miongozo na ilani yake sawa sawa na inavyojinasibu nayo katika Uchaguzi. Swali ni je, Chadema wameachana na lengo kuu la kutafuta kushika madaraka ya nchi na kuunda serikali?Je, Chadema wamekata pumzi na kukubali kucheza ngoma inayopigwa na CCM? Chama cha Upinzani lazima kiwe na ushawishi, Chadema inatakiwa kishawishi wapiga kura kwa kuwa na sera tofauti na chama kinachotawala, tulishuhudia jambo hili wakati wa awamu ya tano ya CCM iliyoongozwa na Hayati Rais John Magufuli, sasa Chadema inayoshirikiana na CCM na kupiga magoti mbele ya viongozi wakuu wa CCM, watatushawishije sisi wapiga kura? Hebu tuongee ukweli tuache uchawa kama alivyosema yeye Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, uhalali wataupataje? hata pumzi ya kudai Tume huru ya Uchaguzi hakuna tena,pumzi ya kudai katiba mpya hakuna tena.
So if they have abandoned the principles, ni kama chama kipya kinachojaribu kujiunda,Hivyo ni bora kibadilishwe jina kabisa na jina la Chadem lipotee au libaki kwa wanaoweza kubaki na ile misingi ya awali ya kuundwa kwake toka 1992 Ni dhahiri CCM nayo inapitia changamoto mpya na ngumu ya kuishi na upinzani kwa kujenga hoja bila chuki, uhasama, kuumiza kuhurumia, kuacha vyombo vya dola visimamie misingi yake na kuachaa kufanikiwa kwenye chaguzi kiupendeleo na kubebwa na mfumo.
Shukrani kwa Rais wetu, Mama Samia kwa kuwa amejitenga nalo sasa wahafidhina hiyo ndiyo kazi ngumu na mtihani wa demokrasia, tumeamua kubadilka na kwenda kwenye utamaduni mpya wa kujenga taifa jipya wengine itawagalimu maana mabadiliko ni magumu, sayansi ya sihasa. Njaa inauma, maharage kilo shilingi 4,500 nyama kilo shilingi 10,000 mchele kilo shilingi 3,700 shilingi yetu inakosa thamani, mkongo au mzambia akija Tanzania na dola 100 atakuja rate ya dola 1 sawa na shilingi 2386 mahesabu yatakuwa hivi 100×2386=238,600 Mtanzania akienda China na Shilingi 10,000 itabidi aibadili kwenda dola halafu aibadili tena kwenda Yuan mahesabu yatakuwa hivi 10,000÷2386×6.8=28.49 tuimarishe uchumi wetu.
Nimalize na Mwenyekiti Ndugu Mbowe, kwa ufupi anasema lengo kuu ni kumsaidia Mama kuongoza vizuri (kwa Tafsiri yangu na nyongeza kidogo ni sawa na kusema lengo sio kushika dola) haya ni maneno yake Mh Mbowe, nanukuu.
"Unafiki na uongo hulaanisha taifa, taifa letu linawatu wengi wasiosema na kuuwishi ukweli, hili ni chimbuko kubwa la mporomoko wa maadili, nakusihi sana mama epuka mtu yeyote anayejiita chawa wako, Mhe Rais sisi wengine tumechagua kusema ukweli, na kukataa dhambi ya unafiki, tumelipa gharama kubwa kwa misingi na misimamo yetu hiyo, tunaamini ukweli, uwazi kutokuwa wanafiki, ndio njia bora ya kukusaidia uweze kuwa kiongozi bora"Mhe.Mbowe (ITV 8.MARCH, 2023). Hili ni jambo jema sio kupinga kila kitu kama mlivyopinga Awamu ya tano ya CCM iliyoongozwa na Hayati Rais Magufuli ambae alikuwa akishughulika na shida za Wananchi kila siku, naamini angekuwepo maharage yasingefika kilo 4,500 Mchele 3,700 sukari 3,400 na nyama kilo 10,000. hii ndio changamoto yenu kwa sasa ila naamini mtaishinda mkiamua.
Copy from chakubanga