Maridhiano ya CHADEMA na CCM yaonesha tobo la kisheria, hayafai hata kidogo

Maridhiano ya CHADEMA na CCM yaonesha tobo la kisheria, hayafai hata kidogo

thetallest

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2017
Posts
8,271
Reaction score
9,113
Katika mjadala wa leo kuhusiana na bandari baadhi ya wachangiaji wengi, kuanzia wa kwanza professor Kitila Mkumbo walionyesha kutoridhishwa na kauli ya muheshimiwa Mbowe ,mwenyekiti wa Chadema taifa,japo hakumtaja jina.

Hali Iliendelea kwa wachangiaji mpaka ikafikia kutajwa hadharani kwamba mlengwa ni Mbowe. Rejea kauli ya Mwita Waitara.

Mbowe kama mtanzania mwingine yoyote yule alitoa maoni yake bila kuvunja sheria za nchi, lakini maoni hayo yamekuwa mwiba kwa watawala.

Nikirejea kwenye maridhiano ya chadema na CCM kumbe hayakuwa ya kisheria bali kishikaji tu na wakati wowote U-turn inaweza kupigwa mwendo ukawa uleule,Ndio ile siri sasa inafichuka taratibu.

Inaonyesha ya kwamba kutolewa kwa Mbowe gerezani kisha kuendelea na mikutano ya hadhara kuna miiko alipewa na CCM.

Mojawapo ni kumsifia rais, kukaa kimya kwa yanayoendelea nchini,kutokukosoa lolote lile, na katika mikutano yao ya hadhara, wasiliguse kwa ubaya jina la Rais Samia, huu ni uzembe wa hali ya juu sana kwa kiongozi mkuu wa upinzani. Hana choice sababu kalamba asali, yuko mtegoni.

Na hii inathibitisha ya kwamba sheria zilizotungwa na Kina Nape Nnauye bado ni valid.ni suala la kufungua faili tu.

Ndio maana leo waziri wa habari na utangazaji katishia kwa kusema kwamba sheria ziko palepale na watadili nao mchana kweupeee.walilegezewa tu kwa mashariti.

Baadhi ya wanachadema walipinga haya maridhiano, waliona mbali lakini walibezwa,sasa matokeo ndio hayo

Kesi ya mwenyekiti faili limefunikwa kwa muda kuangalia mwenendo wake kwa kuwa kalipiwa gharama zote na CCM, tamaa mbaya sana.

Hili ndio tatizo la kulamba asali kimyakimya, imebreakethrough, tutashuhudia mengi zaidi.
 
Nape amekosea Sana Kajionesha anauwezo mkubwa nnchini
Nape ni tatizo kweli,lakini hata upinzani wenyewe ni walegevu sana.

Angalia pia wahariri wa magezeti pia ndio utajua hii nchi ni hopless kabisa.
 
Kuachiwa kwa Mbowe kulimnufaisha Rais Samia sana kwa maana ya kukubalika kimataifa na kupewa misaada na mikopo tele tunayoiona ikijenga mahospitali na barabara.

Misaada na mikopo ya masharti nafuu Mwendakuzimu alinyimwa kwa unyanyasaji wa upinzani.
 
Maridhiano uchwara ni Punguani pekee anayeweza yaamini hayo maridhiano.
 
Kuachiwa kwa Mbowe kulimnufaisha Rais Samia sana kwa maana ya kukubalika kimataifa na kupewa misaada na mikopo tele tunayoiona ikijenga mahospitali na barabara.
Misaada na mikopo ya masharti nafuu Mwendakuzimu alinyimwa kwa unyanyasaji wa upinzani.
Mi najiuliza kosa la Mbowe ni kuuliza bandari ya Zanzibar?
 
Kuachiwa kwa Mbowe kulimnufaisha Rais Samia sana kwa maana ya kukubalika kimataifa na kupewa misaada na mikopo tele tunayoiona ikijenga mahospitali na barabara.
Misaada na mikopo ya masharti nafuu Mwendakuzimu alinyimwa kwa unyanyasaji wa upinzani.
Unalisemeaje onyo alilopewa leo Mbowe na Nnape Nnauye?

Halafu jamaa yangu ni kwambie tu huwezi kutoboa kwa misaada,ni dalili za uvivu uliokthiri
 
Back
Top Bottom