Maridhiano: Zanzibar wanapofanikiwa, Bara tunakwama Wapi?

Maridhiano: Zanzibar wanapofanikiwa, Bara tunakwama Wapi?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Ilikuwa kwenye uzinduzi wa Maalim Seif Foundation ambapo majina mazito mazito pia yalikuwapo.

Walikuwapo kina Samia, Hussein Mwinyi, Othman Massoud, Jussa nk katika wanao matter kwenye siasa za Zanzibar.

IMG_20211106_200104_587.jpg

Hotuba za kusisimua zikitolewa na waliokuwa mahasimu kweli kweli.

Ikumbukwe tumetokea huku:

na watu hawa hawa.

Kama huyu ni Jussa aliyevunjwa bega mwaka mmoja uliopita nini kinashindikana?

Kama hawa ni Othman Massoud na Hussein Mwinyi kishindikane nini chini ya jua?

Kwa hakika vidonda vya Oktoba 2020 vimeonekana kutibika. Bila shaka hata Maalim Seif angekuwapo katika mazingira ya leo, Zanzibar ingekuwa hapa hapa ilipo.

Haiyumkiniki uwepo wa rais JMT ambaye ni mzanzibari kumekuja na Suluhu (mwenyewe) halisi:

Maneno matamu kabisa yenye kuashiria suluhu kamili Zanzibar.

Wakati wazanzibari wakifurahia tamu ya maridhiano kwanini muarobaini huo hautumiki huku kwetu bara?

Kwanini Zanzibar maridhiano ni sasa lakini si huku kwetu bara?

Kwanini kwetu kipaumbele uchumi ni muhimu zaidi lakini siyo huko Zanzibar?

Ni nini siri ya mafanikio ya Zanzibar hali bara kumebakia kizungumkuti haswa?

NB: Maridhiano yoyote Zanzibar hayana chochote cha kufanya na yatokeayo Bara.
 
Kwetu hawataki kwasababu hawana nia hiyo, Mbowe alishaambia kuhusu hilo wakamuona mjinga hawakuhangaika wakati huo huyu mama akiwa kiongozi wa serikali ilitopita.

Wakasema Magufuli alikuwa katili hasikii ushauri wa mtu, ok Magufuli akaondoka, huyu aliekuja akatuambia anatibu majeraha, badala ya kutibu ndio anayaongeza kwa kubambikia watu kesi.

Huku bara ukitaka maridhiano na CCM kwanza ukubali kuwa kondoo wao, ukubali kufanya yote watakayo hata kama ni kukunyima haki zako za msingi kisheria ukubali tu, ukigoma utaitwa mfanya siasa za fujo, then wanatumia polisi wao na mahakama zao kukushughulikia.

Wacha awabebe hao ndugu zake wazanzibari kwasababu wameunganishwa na damu, sisi watoto wa kambo tuendelee kupambana na hali zetu. Anyway, kipimo kizuri cha hayo maridhiano yao ni uchaguzi mkuu ujao, hapo ndio tutajua mbivu na mbichi, ila kwa tabia za CCM ninayoijua mimi...
 
Si mara ya kwanza maridhiano kufikiwa ktk visiwa vya Zanzibar. Utakumbuka wakati wa rais Aman Karume lkn alipokuja Shein nini kilitokea?

Nionavyo mm huu ni upepo wa muda tu.
 
Kwetu hawataki kwasababu hawana nia hiyo, Mbowe alishaambia kuhusu hilo wakamuona mjinga hawakuhangaika wakati huo huyu mama akiwa kiongozi wa serikali ilitopita.

Wakasema Magufuli alikuwa katili hasikii ushauri wa mtu, ok Magufuli akaondoka, huyu aliekuja akatuambia anatibu majeraha, badala ya kutibu ndio anayaongeza kwa kubambikia watu kesi.

Hakuna asiyejua maridhiano ni muhimu. Bila shaka ndiyo maana mama anavutia kwao.

Kwanini kauli hizi ni applicable Zanzibar tu na si bara?
 
Bara tujifunze kwa wazanzibari. Siasa sio uadui. Sisi wote ni watanzania.
 
Hakuna asiyejua maridhiano ni muhimu. Bila shaka ndiyo maana mama anavutia kwao.

Kwanini kauli hizi ni applicable Zanzibar tu na si bara?
Kwasababu wameunganishwa na damu, sisi watoto wa kambo tupambane na hali zetu.
 
Si mara ya kwanza maridhiano kufikiwa ktk visiwa vya Zanzibar. Utakumbuka wakati wa rais Aman Karume lkn alipokuja Shein nini kilitokea?

Nionavyo mm huu ni upepo wa muda tu.

Mkuu, kwani nini kimeyaleta haya sasa?

Angalia uchaguzi Gando ulivyofanyika hadi ukaamuliwa kurejelewa.

Vipi Muhambwe na Ushetu?

Si kuwa ACT Zanzibar baada ya Samia wako vizuri lakini si bara?
 
Bara tujifunze kwa wazanzibari. Siasa sio uadui. Sisi wote ni watanzania.
Unawafahamu CCM? I wish watu wangewafahamu CCM, mnamkumbuka Mwigulu? Mnakumbuka kuwa kuliwahi kua na picha zikimuonyesha akiwa vichakani na vijana? Au mmesahau? Unadhani vile vikundi vya Green guard vimeisha?? Nakumbuka kuna uchaguzi mmojawapo walikua na kambi kabisa Bagamoyo
 
"Sisi sote tumegomboka, kwa ndugu zetu waliopotea.
Walioo, walioipigania hii nchi yetu.
Makusudi, makusudi ya kuikomboa.
Hatusaha, hatusahauu maisha yetu.
Kwa roho, kwa roho zao waliozitoa"
 
Bara tujifunze kwa wazanzibari. Siasa sio uadui. Sisi wote ni watanzania.

Mkuu hudhani kuna mchango muhimu sana kuwa rais JMT kuwa mzanzibari kumeimarisha zaidi Muungano na kuwafanya wazanzibari kuwa wamoja?

Hudhani kuwa iliyokuwa Chatto sasa ni Zanzibar?

Hudhani kuwa inawezekana hawa ndugu wamekubaliana chumbani namna ya kula na vipofu?
 
Unafanyaje maridhiano na kibonde,yaani kwa kura nimekupiga kipigo cha mbwakoko halafu turidhiane,kwa lipi?
 
Si kuwa ACT Zanzibar baada ya Samia wako vizuri lakini si bara?
CCM Zanzibar haijawahi kuwa vizuri kuliko CUF ( sasa ACT). Dola na umafia wa ccm ndiyo uneibakisha madarakani CCM huko visiwani.

Haya maridhiano yatavutugika tu uchaguzi utakapofika. Mgombea urais wa ACT atakapo porwa ushindi wa wazi
 
Uchaguzi ukikaribia ,je maridhiano yatasimama au yatayuka kama barafu juani?
Wazanzibar siku zote wanavurugwa na upande wa bara

Huku Watanganyika hatupendani, ndo maana alipoingia tu madarakani akawatoa wazanzibar wenzake uhamsho, wakati huo huo watanganyika wanamtengenezea mtanganyika mwenzao kesi ya ugaidi na walitaka kumuua Lissu kisa kutofautiana mitizamo ya kisiasa
 
Unafanyaje maridhiano na kibonde,yaani kwa kura nimekupiga kipigo cha mbwakoko halafu turidhiane,kwa lipi?

Refa wewe na mshindani wewe na bado mnao ujasiri wa kujikiia washindi.

Mbona maridhiano haya ni kwa wazanzibari tu? Humuoni Mh. Zitto alivyopwaya kwenye hiyo hafla?
 
CCM Zanzibar haijawahi kuwa vizuri kuliko CUF ( sasa ACT). Dola na umafia wa ccm ndiyo uneibakisha madarakani CCM huko visiwani.

Haya maridhiano yatavutugika tu uchaguzi utakapofika. Mgombea urais wa ACT atakapo porwa ushindi wa wazi

Kwa kuangalia hapa damu ni nzito kuliko maji.

Wazanzibari ambao hawakuutaka Muungano, sasa hivi kimya!

Masheikh wa uamsho na agenda zao, kimya!

Wote wametulizana.

Kwa hali hii inaweza kuwa ni wazanzibari zaidi dhidi yetu na si baina yao.

Bila shaka kama Gando chaguzi huko zitapita kwa haki na salama lakini si Muhambwe na Ushetu.
 
Back
Top Bottom