Ilikuwa kwenye uzinduzi wa Maalim Seif Foundation ambapo majina mazito mazito pia yalikuwapo.
Walikuwapo kina Samia, Hussein Mwinyi, Othman Massoud, Jussa nk katika wanao matter kwenye siasa za Zanzibar.
Hotuba za kusisimua zikitolewa na waliokuwa mahasimu kweli kweli.
Ikumbukwe tumetokea huku:
Your browser is not able to display this video.
na watu hawa hawa.
Kama huyu ni Jussa aliyevunjwa bega mwaka mmoja uliopita nini kinashindikana?
Your browser is not able to play this audio.
Kama hawa ni Othman Massoud na Hussein Mwinyi kishindikane nini chini ya jua?
Your browser is not able to play this audio.
Kwa hakika vidonda vya Oktoba 2020 vimeonekana kutibika. Bila shaka hata Maalim Seif angekuwapo katika mazingira ya leo, Zanzibar ingekuwa hapa hapa ilipo.
Haiyumkiniki uwepo wa rais JMT ambaye ni mzanzibari kumekuja na Suluhu (mwenyewe) halisi:
Your browser is not able to play this audio.
Maneno matamu kabisa yenye kuashiria suluhu kamili Zanzibar.
Wakati wazanzibari wakifurahia tamu ya maridhiano kwanini muarobaini huo hautumiki huku kwetu bara?
Kwanini Zanzibar maridhiano ni sasa lakini si huku kwetu bara?
Kwanini kwetu kipaumbele uchumi ni muhimu zaidi lakini siyo huko Zanzibar?
Ni nini siri ya mafanikio ya Zanzibar hali bara kumebakia kizungumkuti haswa?
NB: Maridhiano yoyote Zanzibar hayana chochote cha kufanya na yatokeayo Bara.
Kwetu hawataki kwasababu hawana nia hiyo, Mbowe alishaambia kuhusu hilo wakamuona mjinga hawakuhangaika wakati huo huyu mama akiwa kiongozi wa serikali ilitopita.
Wakasema Magufuli alikuwa katili hasikii ushauri wa mtu, ok Magufuli akaondoka, huyu aliekuja akatuambia anatibu majeraha, badala ya kutibu ndio anayaongeza kwa kubambikia watu kesi.
Huku bara ukitaka maridhiano na CCM kwanza ukubali kuwa kondoo wao, ukubali kufanya yote watakayo hata kama ni kukunyima haki zako za msingi kisheria ukubali tu, ukigoma utaitwa mfanya siasa za fujo, then wanatumia polisi wao na mahakama zao kukushughulikia.
Wacha awabebe hao ndugu zake wazanzibari kwasababu wameunganishwa na damu, sisi watoto wa kambo tuendelee kupambana na hali zetu. Anyway, kipimo kizuri cha hayo maridhiano yao ni uchaguzi mkuu ujao, hapo ndio tutajua mbivu na mbichi, ila kwa tabia za CCM ninayoijua mimi...
Kwetu hawataki kwasababu hawana nia hiyo, Mbowe alishaambia kuhusu hilo wakamuona mjinga hawakuhangaika wakati huo huyu mama akiwa kiongozi wa serikali ilitopita.
Wakasema Magufuli alikuwa katili hasikii ushauri wa mtu, ok Magufuli akaondoka, huyu aliekuja akatuambia anatibu majeraha, badala ya kutibu ndio anayaongeza kwa kubambikia watu kesi.
Unawafahamu CCM? I wish watu wangewafahamu CCM, mnamkumbuka Mwigulu? Mnakumbuka kuwa kuliwahi kua na picha zikimuonyesha akiwa vichakani na vijana? Au mmesahau? Unadhani vile vikundi vya Green guard vimeisha?? Nakumbuka kuna uchaguzi mmojawapo walikua na kambi kabisa Bagamoyo
"Sisi sote tumegomboka, kwa ndugu zetu waliopotea.
Walioo, walioipigania hii nchi yetu.
Makusudi, makusudi ya kuikomboa.
Hatusaha, hatusahauu maisha yetu.
Kwa roho, kwa roho zao waliozitoa"
Wazanzibar siku zote wanavurugwa na upande wa bara
Huku Watanganyika hatupendani, ndo maana alipoingia tu madarakani akawatoa wazanzibar wenzake uhamsho, wakati huo huo watanganyika wanamtengenezea mtanganyika mwenzao kesi ya ugaidi na walitaka kumuua Lissu kisa kutofautiana mitizamo ya kisiasa