Marriage is an outdated concept

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2020
Posts
9,016
Reaction score
24,650
Sheria ya ndoa imemtasfiri mwanamke wa kizazi cha nyuma kidogo ambae alikua na maadili mema, mtiifu na ana dhamira ya dhati kuidumisha ndoa yake. Kwa sasa wanawake wamejanjaluka na washaona sheria ya ndoa na mahusiano kiujumla ina mianya ambayo inaweza kuwapa pesa/utajiri kirahisi.

Hata wanawake wanaotetea ndoa point zao huwa wanazielekeza zaidi kwenye kuonyesha madhaifu ya wanaume ili ionekane jinsia zote mbili zina shida lakini hapo kwenye upendeleo wanaopewa na sheria mfano kugawana mali ambazo hawanashiriki kuzitafuta huwa hawapagusi.

Kwa mwanaume mwenye ndoto kubwa za kufika mbali kiuchumi basi ndoa ni mtego mkali sana ambao uko mbeleni unaweza kwenda kuiangusha himaya yako uliyoitolea jasho kuijenga kwa miongo mingi.

Kwa mwanamke ambae hana mchango wa moja kwa moja kwenye shughuli za kiuchumi za mwanaume sioni kama ana uhalali wa kupata mgao wa mali baada ya ndoa kuvunjika, hivi mke ambae ni std 7 au o-level failure atatoa mchango gani kuhusu masuala ya tax clearance au business law kwenye biashara zangu?

Kama suala ni kuitunza nyumba na kunipikia chakula je yeye alikua haishi hapo? Alikua hali hapo? Kama mimi natakiwa kufidia muda na jitihada zake kunitunzia nyumba na kunipikiq chakula kupitia kugawana mali mbona mwanamke hawajibiki kunirudishia fidia ya gharama nilizoingia kumpa hifadhi na chakula na matunzo mengine(mavazi, matibabu n.k)?

Kuna watu watakuja hapa kusema vijana tunaona malaya, tunachagua mke instagramu n.k, lakini kumbuka watu wanabadilika hata ukimchukua mke ambae hajasoma uko kijijini sio guatantee ya kusema atabaki ivyo ivyo siku zote.

Hofu ya mustakabali wa maisha ndio umfanya mwanamke aone ndoa ni security kwake. Mwanamke huyu akishapata uhakika wa mustakabli wa maisha yake bila kumtegemea mwanaume basi uona mwanaume ni kikwazo kwake katika kujitawala na hapa ndipo hekaheka zinaanza. Ni wakati wa sheria kumuangalia mwanamke pia kama predator.
 
Evelyn Salt
Unaona lakini tunavyo jitahidi kwenye point, explanation na conclusion

Tunahitaji majibu ya kina kina dada point mbona ziko wazi kabisa jamaangu Ameupiga mwingi.
Ni kweli jamani ndoa ni utapeli, ndoa ni kichaka cha mwanamke kujitajirisha.

Kataa ndoa, fukuza hiyo kausha damu hapo nyumbani
 
Maghayo pasaka haijaisha mshaanza kumalizana

 
A
Ni kweli jamani ndoa ni utapeli, ndoa ni kichaka cha mwanamke kijitajirisha.

Kataa ndoa, fukuza hiyo kausha damu hapo nyumbani
Aah wapi naijua hiyo.. Siwezi kukataa ndoa wakati sijatendwa vya kutendwa na wanawake hata watano.. Ndo kwanza nilianza na kamoja nilikavuta ndani kammakonde kale KAKANICHANGAMSHA FASTA ZA USO ila sijakataa tamaa bado nijaribu Kwanza pengine.

Nitafutie kabinti kamwalimu au nesi nataka nijaribu huko hawa wasio na mishe wanakupiga double yaani hata ya kusuka rasta Zake akutegemee wewe na bado analianzisha anytime... Bora niteseke Na Ka madam changu kamwalimu Nitafutie seriously Tena awe shule za vijijini ili nije kumvuta town uhamisho chap connections tamisemi Ninazo
 
Baada ya miaka mingapi tuje tuwakumbushe ambao hamjaoa juu ya mafanikio mliyopata?

Mtakuja kushangaa fanikio pekee mlilopata ni β€œkutokuoa”

Wazee wote waliozeeka bila kitu haimaanishi hawajawahi kuwa na ndoto. Walijaribu wakajaribu tena na tena na uzee ukafika hawana kitu au walivyonavyo kila mtu anavyo hivyo haviqualify kuitwa mafanikio, just basics.

Ni acceptable kuoa au kutokuoa, ila kusema usipooa moja kwa moja umejiunga kwenye group la mafanikio ni kuwa delusional, na kudhani waliooa wote wataachana na wataflooop kiuchumi nako ni ulemavu wa kufikiri.

On the other hand, Wanawake tunafanya kazi/biashara, na tunamiliki uchumi bila kumjali yeyote.

Cheers πŸ₯‚ tukutane juu.
 
Hata hiyo sheria ya ndoa ikiwa kama kipengele cha kugawana mali ambacho ndio kinawakwaza wengi ikiwa kitaondolewa basi bado sio option ya kufanya wasioipenda ndoa waipende!
Kuna watu sio waoaji wanatafuta visingizio tu! Which is very okay.

Kuna watu hawawezi kuishi na watu, hivyo kuoa kwako ni salama zaidi.

Mali gani? Majaba, masufuria, na sabufa za Alitop? Na plot za 20*20 πŸ˜‚
 
Au sio. Tulia wakupopoe sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…