Binafsi naona siyo sawa kwa Mwanamke aliyeolewa kuwa na rafiki ambaye hajaolewa, vile vile kwa Mwanaume ambaye ameshaoa kuwa na rafiki “muhuni” ambaye bado yuko single, ni vizuri wenye ndoa wakawa na marafiki wa pia wenye ndoa, angalau inaweza kusaidia kuokoa ndoa.
Lkn wakati mwingine unakuta Mwanamke kaolewa lkn ana rafiki single kutwa anashinda viwanja, sasa wanaongea nini?
Sijaolewa ila naexperience yakuishi na mtu .
Kuolewa ni kitu chema na ukishaolewa unabadilika naunakuwa na majukumu na upo busy masaa yote .
Kabla hujapata mtoto unamume wakumtunza na kumuhudumia naunaenda home mapema kabla yake kumuandalia chakula na kuweka nyumba safi wewe nawe uwe msafi .
Kingine mume wako unatakiwa kumuona special nakumjali.
Lazima kila siku uwe kwa ajili yake.
Ila mwanaume naye pia lazima awe tayari kuhudumiwa ,kushukuru , kupenda nakujali nakuwa tayari kuitwa baba /mume na mpenzi sasa anatakiwa naye ashiriki katika kufanya usafi , kupika na kuwa tayari kwa usaidizi wowote wa nyumbani sio kujibweteka tu nakusubiria tu mwanamke amfanyie kila kitu .
Kwanini mwanamke anarudi kuwa single ni ushirikiano hakuna mwanaume haoni au hajajianda kuwa mume anarudi usiku muda wakula umepita na juhudi ya mwanamke wake inapotea mtu anafanya siku kadhaa anaona ajichanganye na masingle ladies kunirusha arudi muda mume wake karudi so wanarudi wote .
Kila akiboreka inambidi afanye hivyoo ili asiboreke .
Maisha ya ndoa nikujitoa sio kuishi nje ilimradi uwe na pete mkononi hapa ni matendo nimeoa au nimeolewa haupo tena single unaenda kwa mwenzi wako kama hukuwa tayari usingeoa .
Kuna wanawake ni wakubwa 38 au 40 ila bado hawaoni kuwa wameolewa watulie home hapana wanazurura zurura kama matahira hawatulii.
Hata wanaume wengine wakioa wapo hivyoo hawapo serious na ndoa wanashinda bar na huku kaacha mke home good day