Mwananchi wa chini
JF-Expert Member
- Jul 23, 2013
- 227
- 599
1. Alizaliwa Tarehe 15 Januari 1929, Atlanta Georgia nchini Marekani na kufariki Memphis April 4, 1968. (Aliishi Miaka 39)
2. Baada ya kuzaliwa alipewa jina la Michael King Jr , Baba yake aliitwa Michael King Sr(senior) ila Lilibadilishwa na kuwa Martin Luther King, Baada ya Mwaka 1931 baba yake mzazi kutembelea nchini Ujerumani na kuvutiwa na Mhubiri anayeheshimika kama mtu wa Matengenezo ya kanisa kurudi kwenye Misingi yake ; Martin Luther King aliyehasi Katoliki.
3. Martin Luther King Jr ni miongoni mwa watu watatu wanaopewa heshima ya kitaifa (Federal Holiday); katika majimbo yote 50 yanayounda taifa la Marekani. Watu Wengine waliopewa heshima hiyo ni "mpelelezi na mvumbuzi" Christopher Columbus na George Washington Raisi wa kwanza wa Marekani. Suala la kutambua MLK DAY kama Federal holiday Lilipitishwa na Bunge na kuwa sheria katika taifa la Marekani baada ya kusainiwa na Raisi Ronald Reagan Mwaka 1983, ikaanza kutekelezwa miaka mitatu baadae. Baadhi ya majimbo yalikuwa yamekataa kuitambua siku hiyo na mengine yaliunganisha na siku nyingine, lakini kufikia mwaka 2000 majimbo yote 50 yalikubali na kuifanya rasmi kuwa sikukuu ya kitaifa.
4 . Martin Luther King Jr akiwa na miaka 12 alifanya jaribio la kujiua kupitia dishani kutoka ghorofa ya pili na kujitupa chini kutokana na msiba wa kuondokewa na Bibi yake aliyempenda sana , aliyekufa kutokana na mshutuko wa moyo. Hata hivyo alipona majeraha yake baada ya muda mfupi.
5. Akiwa mwanafunzi "aliruka" madarasa mawili (darasa la tisa na darasa la 11) kutokana na ufahamu wake kuwa mkubwa.
6. Alihitimu shahada yake ya kwanza katika Sociology akiwa na miaka 19 tu na akapata shahada ya Uzamivu (PHD in systematic Theology) akiwa na miaka 25.
7. MLK Jr hakupenda kuwa Mchungaji na hata baada ya kuhitimu masomo yake, alimwambia baba ya MLK Sr kwamba hakutaka kuwa mhubiri badala yake alitaka kuwa Daktari au Wakili Msomi!
8. Miaka 10 kabla ya kifo chake yaani Tarehe 20 September 1958 , aliponea kufa baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali na mwanadada Izola Ware Curry, wakati akisaini nakala za kitabu chake kipya cha "STRIDE TOWARD FREEDOM" baada ya kusema yeye ndie MLK Jr, mtu huyo alidai alikuwa anamtafuta kwa miaka mitano, mara ghafula mtu yule akamchoma na kitu cha ncha kali kifuani hata hivyo alikimbizwa hospitali alisaidiwa na madaktari kwa upasuaji uliochukua saa kadhaa.
9. Alikuwa anavutiwa sana na mwanamageuzi Mahatma Ghandi wa India kutokana na Falsafa ya kuhitaji mapinduzi bila machafuko (Non-Violence Movement).
10. Alipendekezwa na kushinda Tuzo ya Time Magazine ya Man of the Year na kuwa mtu mweusi wa kwanza kushinda tuzo hiyo mwaka 1964 ikiwa ni kwa ajili ya mwaka ulioisha 1963.
11. Mpaka sasa ndie MWANAUME Mwenye umri umri mdogo kushinda Tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1964 akiwa na miaka 35. MTU mwenye umri mdogo kuwahi kushinda Tuzo hii ni Mwanadada Malala Yousafzai aliyeshinda Tuzo hiyo mwaka 2014 akiwa na Miaka 17.
12. MLK Jr baada ya kushinda Tuzo hiyo na kupata fedha hizo $54,123 ambayo kwa sasa ingekadriwa kuwa $400,000; Fedha zote hizo alizielekeza katika Vuguvugu alilokuwa analiongoza na kupinga ukandamizwaji wa haki za mtu mweusi akishirikiana na wahubiri Billy Graham na Ralph Abernathy na wengineo.
13. Mwaka 1971 Jina lake lilichaguliwa na kushinda tuzo ya Grammy ; Medali ya heshima ya dhahabu ya Congress (Congressional Gold Medal) na medali ya Uhuru (The medal od Freedom) na alishinda medali hizo kutokana na kupinga Vita ya Vietnam na Marekani.
14. Mama yake aliyeitwa Albertha Williams King naye pia aliuawa akiwa amehudhuria kanisani huko Atlanta na kijana wa Miaka 23 alisema kwamba aliamini kwamba "Wakristo wote ni maadui" kwa hiyo aliona vema kumuua mama Albertha.
15. Takriban mitaa mia tisa (900) katika Marekani yote inaitwa Martin Luther King Jr kwa heshima yake.
16. Martin luther king Jr alikamatwa na kuwekwa jela takribani mara 30 katika uhai wake na kosa kubwa ilikuwa kupinga uonevu na unyanyasaji waliokuwa wanafanyiwa watu weusi nchini Marekani na ulimwenguni kote hususani Ulaya ,Amerika ya kusini na Amerika ya kasakazini.
17. Martin Luther King Jr alikufa kwa kupigwa risasi na mtu aliyeitwa James Earl Ray tarehe 4.4. 1968 ikiwa ni siku moja baada ya kutoa hotuba ya "I HAVE BEEN TO THE MOUNTAIN TOP" ambayo ni kama aliona mwisho wake; maana kesho yake ndio siku aliyouwa kwa kupigwa Risasi akiwa ubarazani kwenye hotel iliyoitwa, Lorraine Motel.
18. Uchunguzi wa FBI kuhusu kifo chake umebaki siri na utatolewa ifikapo mwaka 2027, kutokana na mkanganyiko wa tukio na wahusika wake. Ingawa ni mmoja alikamatwa na kuhukumiwa kwenda jela. Miaka kadhaa imepita mtu mmoja aitwaye Loyd Jowers alijitokeza na kusema alihusika na shambulio la kumuua MLK Jr na walishirikiana na Serikali pamoja na Mafia kutekeleza Shambulio hilo.
19. Hotuba yake ya I HAVE DREAM " imebaki kama moja ya hotuba mashuhuri katika historia ya Marekani; na anakumbukwa kwa yeye pamoja na viongozi wengine kuratibu maadamano ya mwaka 1963 (Washington March) yalipelekea kutungwa kwa sheria mpya ya kupinga unyanyasi na ubaguzi katika utoaji kazi na huduma za jamii kwa watu wote. (CIVIL ACT 1964).
Mabaya yake hayakosekani lakini mema yake mengi yanatupa ujasiri wa kujifunza baadhi ya mambo katika maisha yake kwa faida ya kizazi tulicho nacho .