Hao ni watu muhimu sana katika historia ya mtu mweusi mmarekani, Malcolm na Luther waliokuwa na tofauti kubwa juu ya nama ( means) ya kufikia lengo kuu yaani watu weusi kupata haki zao. King jr alikuwa anaamini katika njia amani kupata haki, wakati Malcolm alikua anaamini katika njia yoyote inayohitaji "any means neccessary" na msemo wake maalumu ni haki haiombwi bali inachukuliwa, right is not given, is taken. Pia King jr alikuwa anaamini katika greater Americanism, yaani marekani ya wazungu na weusi, Malcolm alikua haamini kama mtu mweusi anaweza kupewa haki na mtu mweupe hivyo njia pekee ni weusi kuunda taifa lao( black separatism). Katika muktadha wa Kiafrika King jr alikuwa anaamini katika umoja wa wamarekani, Malcolm yeye alikuwa anaamini katika umajumuhi wa kiafrika yaani pan africanism