Martin Masese: Festo Kiswaga jimbo la Kalenga ni mfano mmoja tu wa wabunge mzigo, wa kupewa vimemo na kujiropokea

The Palm Beach

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
4,249
Reaction score
11,592

HUYU NDIYE MMOJA WA WABUNGE MZIGO. ANAPEWA KIMEMO NA MAFISADI WAKIONGOZWA NA KENANI KIHONGOZI KWA UJIRA WA 1M NYONGEZA YA POSHO YAKE YA SIKU, ANAFYATUKA BILA KUSHUGHULISHA KICHWA CHAKE KWA KUFANYA UTAFITI MDOGO TU NDIPO APANUE DOMO LAKE KUSEMA ​

Mtu ‘anayejiita mbunge’ anasema Serikali ya CCM imeongeza bei kidogo sana ya mafuta kulinganisha na Kenya. Huyu mtu hajajishughulisha vya kutosha.

Huwezi kulinganisha uchumi wa nchi na nchi kwa kutaja tarakimu tu. Kulinganisha uchumi wa Tanzania na Kenya anatakiwa kutumia vipimo viwili vikuu ambavyo ni;

GDP per Capita (Pato la Taifa kwa kila kichwa) na GDP per Capita PPP (Pato la Taifa kwa kuzingatia Uwezo wa Kununua - Purchasing Power Parity). Zingatia hivyo.

1.GDP Per Capita (Nominal); Hiki ni kipimo cha thamani ya fedha ya bidhaa na huduma zote zinazozalishwa nchini, ikigawanywa kwa idadi ya watu katika nchi.

GDP (pato la Taifa) inatumia viwango vya soko vya kubadilisha fedha (USD). Hii hutumia viwango vya soko vya kubadilisha fedha (market exchange rates).

Tofauti na Tanzania ambayo uchumi wake unategemea zaidi rasilimali za asili (kama madini), Kenya imejenga msingi wake katika sekta ya huduma na ubunifu.

Kenya ni kiongozi wa kidijitali barani Afrika, jambo lililoipa jina la utani la “Silicon Savannah.” Mapinduzi ya huduma za kifedha kwa njia ya simu yalianzia hapa.

Nairobi ni makao makuu ya makampuni makubwa ya teknolojia duniani (Google, Microsoft, na Amazon) yanayofanya shughuli zake katika bara la Afrika.

Benki za Kenya (kama Equity na KCB) zimepanuka na kutawala soko la kanda ya Afrika Mashariki na Kati, zikiwa na matawi nchini DRC, Rwanda, South Sudan

Uchumi wa Tanzania kwa sasa unapitia kipindi cha mpito ambapo matokeo yake katika thamani ya sarafu na soko la kimataifa yanachukua muda sana kuonekana.

Tanzania inasafirisha madini ghafi. Thamani kubwa ya soko inabaki nchi za nje ambako madini hayo yanasafishwa na kutengeneza bidhaa za mwisho.

Thamani halisi inayobaki ni asilimia ya mirahaba na kodi, wakati thamani kubwa ya soko la madini hupimwa masoko ya hisa ya kimataifa (London au Toronto).

Uchumi wa Tanzania una sehemu kubwa sana ya sekta isiyo rasmi inayozalisha fedha nyingi, lakini hazionekani kwenye takwimu rasmi za thamani ya soko la kidunia.

Kwa wastani, raia mmoja wa nchi ya Kenya anaonekana kuzalisha thamani ya fedha karibu mara mbili ya raia mmoja wa Tanzania katika soko la kimataifa.

2.Purchasing Power Parity (PPP); Hiki ni kipimo cha “uwezo wa kununua.” Kinarekebisha tofauti za gharama za maisha na bei za bidhaa kati ya nchi hizi mbili.

Kwa mfano, kama $1 inaweza kununua mikate miwili Tanzania lakini kwa bei hiyo, unaweza kununua mkate mmoja tu nchini Kenya, PPP inazingatia ukweli huo.

Kenya ina kipato kikubwa, gharama za maisha ni kubwa. Tanzania ina gharama ndogo za maisha baadhi ya sekta (vyakula vya asili na baadhi ya huduma za kijamii).

Kenya ina sekta ya huduma (Banking, Tech, Tourism) iliyoendelea zaidi, ambayo huzalisha thamani kubwa ya fedha. Tanzania inategemea zaidi Kilimo na Madini.

Kenya imekuwa kitovu cha kibiashara (Regional Hub) kwa muda mrefu, jambo linalovutia makampuni mengi ya kimataifa kufanya uwekezaji mkubwa Kenya.

Kwa sasa nchini Kenya, bei za mafuta zilizotangazwa na Mamlaka ya Kudhibiti Nishati na Petroli (EPRA) zinazotumika hadi Aprili 2026 kwa Mombasa;

Petroli (Super Petrol) KSh 189.60 kwa lita (Tsh3,771. Dizeli (Diesel) KSh 173.10 kwa lita (Tsh 3,452). Mafuta ya Taa (Kerosene) KSh 163.00 kwa lita (Tsh 3,253).

Hizo habari lita moja ya mafuta ya petroli Kenya inauzwa Tsh 5,450 ametoa wapi? Au amesogezewa kipeperushi na KIHONGOSI kutoka ma’group yao ya WOSAPU?

Mtu ambaye anayejiita ‘mbunge wa CCM’ alitakiwa apitishe ubongo wake maeneo hayo, halafu ajenge hoja zake. Vinginevyo ni MPUMBAVU mwenye ujasiri.

 
Hapa Kenya kila bus na nauli yake lakini Tanzania matapeli wanataka kuwapangia watu nauli za gari zao😭
 
Huyu jamaa alikuwa Zonal Director wa Tigo zone ya South,mikoa ya Iringa,Mbeya,Ruvuma na Rukwa...alikuwa anajenga hoja vizuri sana,sijui kapatwa na nini...yawezekana wameshajua boss wao anapenda watu wajinga
 
Huyu jamaa alikuwa Zonal Director wa Tigo zone ya South,mikoa ya Iringa,Mbeya,Ruvuma na Rukwa...alikuwa anajenga hoja vizuri sana,sijui kapatwa na nini...yawezekana wameshajua boss wao anapenda watu wajinga
Ndio ile insyosemwa, ukiwa nje ya CCM mtu huwa timamu na akili zake...

Lakini ukikimbilia na kujiingiza ndani ya CCM ili kujipatia maslahi cheap ya kiwiziwizi, papo hapo unakuwa zoba, akili zinachukuliwa na wachawi na waganga wao wa kienyeji, mtu anabaki kopo tu..!
 
Huyu jamaa alikuwa Zonal Director wa Tigo zone ya South,mikoa ya Iringa,Mbeya,Ruvuma na Rukwa...alikuwa anajenga hoja vizuri sana,sijui kapatwa na nini...yawezekana wameshajua boss wao anapenda watu wajinga
Well joined ccm , his brain na kila kitu akaacha nje. Mtu anatoka kuwa southern zonal director, why kuitupa career yako na kwenye kujichafua kwenye politics?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…