Marudiano na Burundi Ndairagije apewe likizo

Team JPM

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2018
Posts
1,197
Reaction score
1,826
Nikweli kwamba kocha ni mwajiriwa na anapaswa kuisaidia timu iliyomwajili kupata usjindi, Shaka la mgongano wa kimaslahi haliepukiki
Katika mechi za vilabu sio rahisi lakini kwa timu za Taifa sio salama sana. Kwa tunavyowafahamu majirani zetu, wao ni Taifa kwanza alaf maslahi binafsi baadae.. Nikweli kwamba hatujafikia viwango vya kupeleka timu kwenye kombe la dunia lakini hatupaswi kutolewa na Burundi. Tutoke mbele ya safari lakini sio kizembe hivi. Sio rahisi kocha wetu mpendwa RAIA wa Burundi akaiondosha mashindanoni timu ya nchi take. Ili kuondoa hisia za hujuma, kocha huyo apumzike hadi mechi ya marudiano ipite. Ili Hata tukitolewa basi tusimshutumu kutokana ns mgongano wa kimaslahi.
Mfano Dhahiri ni Haruna Shamte kuushindwa mchezo lakini kocha akamnyamazia wakati kuna Hassan Kessy na Shaibu. TFF huu ni ushauri wa kizalendo kabisa na utamuweka huru kocha wetu
 
Kuanzia na shamte, Hemedy Mao pamoja na Gadiel wakati nje kuna kina Kessy, Farid Mussa, Zimbwe Junior uko ni kutuujumu mchana kweupe. Sikatai kwamba sio kocha bora ila Utaifa unasumbua watu wengi ata ningekuwa mm ningewaujumu nje ndani.
 
Nyie Watanzania ni watu wa ajabu sana. Huo pia ni mwanzo wa ubaguzi.
Huyu kocha alitaka kumwingiza Kesi, lakini baada ya kupigwa goli moja akaona hapana akabadili gia akamuingiza. Faridi Musa. Hapo kocha alifnya jambo la maana ili kuongeza mashambulizi mbele.
Nani kati yenu amemfuatilia Hasan kesi kwa mechi za hivi karibuni.
Kesi na Shabalala ni wazuri Kwenye kushambulia lakini si wazuri kurudi kukaba.
Wakikutana na yule mrudi wa Jana aliyeingia kipindi cha pili kule kwa shamte akina Yondani watapata kazi kubwa zaidi ya waliyopta kwa kuwepo shamte.
Siseme Shamte hana makosa. Lakini kwa mchezo wa ugenini Game plan ya kocha ilifanikiwa
 
shamtealicheza vizuri sana ila tunachoshindwa kuelewa ni kwamba alikuwa anacheza na mtu mwenye weledi wa soka. ni mjanja na mwepesi kumtoka beki in short jamaa yule anaujua mpira vizuri. ila kumbukenei angekuwa anacheza na hassan kessy game tungepigwa kwa sababu kessy angetolewa kwa kadi nyekundu mapema sana. kwa sababu asingeweza kumkaba yule jamaa kistaarabu na kwa akili kama alivyokuwa anafanya shamte. kessy sio mvumilivu wa kupigwa vyenga mara kwa mara.
 

Naomba tu nitofautiane na wewe. Huyo Haruna Shamte anaweza akawa ni mchezaji mzuri! Ila hawezi kulingana ubora na uzoefu, na mtu kama Shomari Kapombe au Hassan Kessy! Tukubali tu ukweli, mechi ya jana ilimzidi nguvu. Bila shaka anahitaji muda zaidi wa kujifunza kwa hao niliowataja.
 
Wewe ndio unajua mpira mleta mada ni mjinga moja anaendeshwa na mihemko badala ya uhalisia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…