Marudio ya Hamza Kassongo on Sunday Jumamosi 2 Januari 2021 saa tisa mchana anazungumza na Mohamed Said

Marudio ya Hamza Kassongo on Sunday Jumamosi 2 Januari 2021 saa tisa mchana anazungumza na Mohamed Said

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
HAMZA KASONGO ON SUNDAY MAZUNGUMZO NA MOHAMED SAID KITARUDIWA JUMAMOSI 2 JANUARI 2021 SAA TISA MCHANA

Marudio ya "Hamza Kassongo on Sunday," TVE kitarushwa In Shaa Allah Jumamosi ijayo saa tisa mchana mada ni "Mchakato wa Uhuru."

Kipindi cha saa nzima tunazungumza historia ya kujikomboa kwa Tanganyika kuanzia African Association 1929 hadi kuundwa kwa TANU 1954.

Utapata fursa ya kusikia historia ya wazalendo ambao hawafahamiki sana katika historia ya uhuru wa Tanganyika kama Hamza Kibwana Mwapachu, Rashid Ali Meli, Ali Mwinyi Tambwe, Iddi Faiz Mafungo, Robert Makange na Rashid Kheri Baghdelleh, Chief David Kidaha Makwaia, Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Hawa bint Maftah, Earle Seaton, Schneider Plantan na wengine wengi.

1609532690895.png
1609532737036.png
 
Kumbe yule ndio wewe? Yaani Mohamed Said?

Nilifurahi sana kuangalia yale mahojiano na nimekuja kugundua hapa JF tunabishana na watu ambao pengine tungetulia tungepata maarifa makubwa mno. Kipindi kizuri sana nilikuwa nahitaji kitabu chako ambacho ulisema pale kuwa historia ya Uislam machame.

Mungu azidi kukupa umri mrefu na tupate nasaha zako.
 
Desemba 28, 2020
Part 1

HAMZA KASSONGO ON SUNDAY MCHAKATO WA UHURU

Umahiri wa Sheikh Takhadiri, Bibi Titi na Mwalimu Nyerere ktk kuhutubia. Jinsi wasomi wa TANU walivyowachochea makabwela kushiriki kwa wingi ktk siasa. Mtambo wa uchochezi wa TANU uliowakera Waingereza waliokuwa na mamlaka.


Source : mohamed said
 

December 28, 2020

Part 2​

HAMZA KASSONGO ON SUNDAY MCHAKATO WA UHURU 2

Nyerere achaguliwa kwa ushindi wa kura chache dhidi ya upinzani wake wa karibu kuongoza TANU



Source : mohamed said
 
December 28, 2020
Part 3

HAMZA KASSONGO ON SUNDAY: MCHAKATO WA UHURU 3
Dua alizofanyiwa Mwalimu Nyerere na wazee wa Bagamoyo.....


Source : mohamed said
 
Nchi hii kuna watu wengi wamekifanyia mambo makubwa TANU/CCM zamani na familia zao zipo wazetelekeza,alafu sahvi kuna mijitu inajifanya wanaijua nchi hii sanaa
Kama utapata wasaa tupe historia ya sheikh rahamia,said TANU
Mohamed Said

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom