1.askofu yupo sahihi kabisa.
2.kuachana kupo iwe kwa mujibu wa biblia au sheria ya ndoa ya mwaka 1971.
3.pamoja na labda makosa makubwa aliyotenda mkeo,mwanamume inabidi tuwe na roho ya kiutu na kibinadamu.
4.pamoja na kuwa unakila uhakika kuwa mimba si yako,lakini bado utu unahitajika.kiumbe wa tumboni hana kosa lolote,
kwa nini unamwadhibu?ni ushetani huo.
5.ni vema na ni busara ukakaa kimya na kuvumilia, mkeo/mpenzi wako akishajifungua mtoto, sasa waweza kuanzisha mipango ya talaka,hapo hata mungu atakuwa upande wako(hasa ikiwa mnaachana kwa ajili ya zinaa ya mkeo)
6.pamoja na hayo jamii nzima itakuona wewe mwanamme mwenzangu hufai ukimwacha mkeo ili hali mjamzito,watasema kazi yako ni kujaza mimba na kukimbia.na ikitokea mkeo
akakuchomekea kuwa kanikimbia kwa vile nina mimba....umekwisha kila mtu atamuunga mkono na kukulaani wewe kumbe kosa ni lake mkeo, huenda kazini na kupewa mimba labda na house boy wako.subira na busara ni muhimu tuache hasira,siku zote hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu....biblia inasema hivyo.