Marufuku kubeba petroli kwenye vidumu

sasa kama nataka kusafiri safari ndefu na inanilazimu nibebe mafuta ya ziada ndio nafanyaje?

Hapo ndipo tunapoona kuwa nchi haina viongozi wanaofikiria beyond their own interests. Ningekuwa mimi ni muhusika ningesema mtu asiuziwe mafuta kwenye kidumu mpaka aoneshe kadi ya gari au aje na gari kituoni au aoneshe leseni au risiti ya kumiliki chombo kinachotumia mafuta ambacho hakiondosheki. Ukweli ni kwamba sheria hii ya kijinga inatekelezwa na wenye vituo kwa sababu inawapatia mwanya wa kuwaibia wananchi through faulty pumps. Kamaa ingekuwa inawabana wasingeitekeleza asilani. Nafikiri wahusika wanatakiwa kuja na tamko jipya kuhusu huu upuuzi. Maamuzi ya kukurupuka ni mabaya sana, walitakiwa kufanya utafiti kwanza wa kwa nini wtu hutumia vidumu?. Je kuna petrol stations za kutosha kwenye barabara kuu?, halafu wajiulize je kuna usalama katika barabara kuu kwa mtu kutembea na kiasi kikubwa cha pesa ili kununulia mafuta?, majibu yote haya ndiyo yangepelekea kuana na maamuzi sahihi.
 

Niliudhika juzi kiasi cha kutaka kumwaga matusi ya nguoni kwa wauzaji mafuta, Umeme wa mgao, mimi nimeshasahau kuhusu Tanesco ninakijenereta changu miaka nenda rudi, nafika kituo cha mafuta eti kidumu hakiruhusiwi, mbaya zaidi siku hiyo kulikuwa na msiba hivyo tulihitaji sana mwanga hivyo genreta ndiyo ilikuwa mkombozi wetu! Sasa jamani hivi viongozi wetu wanachowaza kwa watanzania wa hali za chini ni kuwaudhi na kuwaumiza tu!! Mbona hivyo jamani? mbona mna mambo ya..............mbu, ......zenu........wako@******##$$&&& sitaki hata kutamka hayo maneno kwa kujali maadili ila kama tungekutana ana kwa ana bila ushahidi anangejuta huyo mwenye mawazo ya kuzuia vidumu.
 
Na sisi ambao tunaishi vijijini umbali wa kilomita 50 toka mjini itakuwaje? manake huko kwetu abiria wanasafirishwa ktk malori ambayo yamebeba madumu ya mafuta ya dizeli kwa ajili ya mashine za nafaka,sheria inasemaje?
 
"Wenye majenereta na mashine za nafaka wazibebe mpaka Petrol Station...."

Mwisho wa kunukuu....
 

Licha ya kukuta mafuta hakuna petrol station, foleni tu za mjini zinaweza kupotezea timing.
 
Chupa ya plastiki ndio vidumu????????????? mbona chupa ni chupa dumu ni dumu na material yanayotengeneza dumu sio yanayotengeneza chupa za plastic. Labda mtoa hoja ajikague tena, vituo vya mafuta wanakaataa chupa za plastic na sio madumu bana.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…