Marufuku kunywa pombe asubuhi Singida

Marufuku kunywa pombe asubuhi Singida

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau hamjamboni nyote?

#HABARI Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amepiga marufuku wananchi wa mkoa huo kuanza kunywa pombe asubuhi badala ya kufanya shughuli za maendeleo na za kiuchumi hali ambayo inaweza kusababisha kudumaa kwa shughuli za kiuchumi kwa wananchi.

Mkuu wa mkoa ametoa kauli hiyo leo Aprili 19, 2024 katika Kijiji cha Kashangu, Halmashauri ya Itigi kwenye ziara yake ya kikazi ya siku mbili kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo ya Elimu na Afya (PAUSE)

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa mkoa huo, Dkt. Fatma Mganga amewataka watendaji wa halmashauri na kata kusimamia vizuri ujenzi wa miradi ya maendeleo hasa umaliziaji wa majengo mbalimbali ili kudhibiti vitendo vya wizi wa vifaa vya ujenzi.

Amesema hatapenda kusikia wala kuona wizi wa vifaa katika miradi ya maendeleo hivyo Viongozi lazima wasimamie kikamilifu utekelezaji wa miradi hiyo ili iweze kuleta manufaa kwa Wananchi na sio vinginevyo.

1713547032522.jpg
 
Mtu mwenye shughuli zake hawezi kuacha kuzifanya akaenda kunywa pombe,ukiona mtu anakunywa pombe asubuhi basi ujue keshamaliza kazi zake au hana kazi ya kufanya na hela anayo hivyo viongozi waache kujifanya manyapala kwenye maisha ya watu.

Wao wadhibiti watumishi wao wasiingie kazini wakiwa na kilevi na atakayekwenda kinyume achukuliwe hatua za kinidhamu lakini sio kupangia kila mtu kwa sababu kila mtu ana njia zake za kupata pesa na yeyote atakayebainika ni mhalifu hatua za kisheria zifuate mkondo wake vinginevyo kila mtu ashinde mechi zake.
 
Wadau hamjamboni nyote?

#HABARI Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amepiga marufuku wananchi wa mkoa huo kuanza kunywa pombe asubuhi badala ya kufanya shughuli za maendeleo na za kiuchumi hali ambayo inaweza kusababisha kudumaa kwa shughuli za kiuchumi kwa wananchi...
Kheri anayekunywa pombe asubuhi kwani anaingiza mapato serikalini kuliko yale makundi ya vijana machokoraa wanaozurula nao kila siku ili wawashangilie na kukata viuno kwenye mikutano yao.
 
Loooh maisha ya Iran sasa.
 
Mtu mwenye shughuli zake hawezi kuacha kuzifanya akaenda kunywa pombe,ukiona mtu anakunywa pombe asubuhi basi ujue keshamaliza kazi zake au hana kazi ya kufanya na hela anayo hivyo viongozi waache kujifanya manyapala kwenye maisha ya watu.
Wao wadhibiti watumishi wao wasiingie kazini wakiwa na kilevi na atakayekwenda kinyume achukuliwe hatua za kinidhamu lakini sio kupangia kila mtu kwa sababu kila mtu ana njia zake za kupata pesa na yeyote atakayebainika ni mhalifu hatua za kisheria zifuate mkondo wake vinginevyo kila mtu ashinde mechi zake.
Na kingine. Nchi haiongozwi kwa matamko ya majukwaani. Nchi ina sheria. Bar zinajulikana zinafunguliwa saa ngapi. Maduka ya kuuza pombe nayo hivyo hivyo. Badala wajenge mifumo wao wanakazania kupanda majukwaani kugeuka sheria.
 
Back
Top Bottom