Marufuku ya vifungashio vya plastiki: Nawaza hivi mikate ya slice itafungashwa kwenye nini na bidhaa nyingine kama korosho nk

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti la mwananchi leo nimeona tangazo la OMR Muungano na mazingira kuhusu mwisho wa matumizi ya vifungashio vya Plastiki kama vibebeo.

Akili yangu ikajiuliza fasta fasta hivi ile mikate maarufu ya slesi ambayo tulikuwa tunabeba kupelekea ndugu zetu vijijini kama ishara kuwa umetoka Dasalamu itafungashwa kwenye vibebeo gani?
 
Mie mwenyewe hiyo mifuko nimeshangaa mwezi ulopita kuambiwa haitakiwi nayo tena!... mh
 
Mkuu naona umesoma kwa kukurupuka hio taarifa, au umesikiliza redioni wakikusomea.

Taarifa inasema mifuko ya plastiki kwa ajili ya kufungashia chakula haijapigwa marufuku bali inapaswa ikidhi viwango vya tbs!

Siku nyingine uwe unasoma taarifa kamili sio kukurupuka kufungua nyuzi kwa kila kitu bila na kuwa na taarifa kamili.
 
Ipo mifuko ya plastiki inayooza,iyo ndo inayotakiwa kufungashia iyo mikate yako unayosema.
 
Topic closed...
 
Watoe mbadala wake kabla ya kufunga
 
Kukurupuka maana yake nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…