Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Mary ameenda kutoa onyo hilo huku akiwa mgeni mresmi wenye hafla ya kutoa 'zawadi' kwa wananchi, si ndio yale yale ama? Au ukiongozana na kiongozi mwingine ndio inaacha kuwa rushwa?
=====
Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Pius Chatanda (MCC) amekasirishwa na tabia ya baadhi ya wanasiasa wanaotafuta uungwaji mkono kwa Wajumbe kabla hata ya kuanza rasmi kwa zoezi hilo kwani inadhorotesha juhudi za utekelezaji wa Ilani ya CCM zinazoendelea kufanywa na viongozi waliopo madarakani.
Chatanda, ametoa onyo kali kwa Wabunge na Madiwani wanaowasaidia wale tu waliowawezesha kukalia nafasi hizo.
Onyo hilo limetolewa 20 Disemba, 2024 Mkoani Ruvuma akiwa ni mgeni rasmi katika hafla ya kugawa vitendea kazi mbalimbali ambazo ni mashine za kukamulia alizeti, vyerehani, majiko ya gesi, Ng'ombe wa maziwa, Baiskeli kwa mlemavu na Mifuko ya Saruji kwa makundi mbalimbali Mkoani Ruvuma.
Pia soma: Kuelekea 2025 - Chatanda Kuchangia Mifuko 50 ya Saruji na Pesa Milioni Moja Gereza la Mbozi - Songwe
Aidha, Chatanda amepiga marufuku kwa Makatibu UWT Mikoa na Wilaya Wanaowatisha Wabunge ili wawapelekee zawadi ya pesa na vitenge jambo ambalo amesema ni kinyume na nafasi zao wanazozitumikia.