Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mary Masanja amesema Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imejipanga kuboresha huduma kwa watalii katika nyanja mbalimbali ili kuvutia watalii wengi zaidi ikiwa ni mkakati mahsusi wa kuwafanya watalii ho kuongeza siku za kukaa nchini na hatimaye kukuza pato la Taifa.
Mary Masanja ameyasema hayo tarehe 23 Machi, 2023 katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kilichofanyika jijini Dodoma.
Moja ya mkakati wa Serikali ni kuboresha huduma za Malazi kwa watalii pamoja na kuzirejesha hoteli za Wizara ambazo zilikuwa zinaendeshwa na Sekta binafsi ambazo kwa ujumla wake hazifanyi vizuri.
Serikali ina mkakati wa kuboresha maeneo ya fukwe na kuunganisha vifurushi vya safari za watalii. Vile vile Serikali kupitia Wizara husika itaendelea kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii pamoja na kufanya utafiti wa kujua vivutio vipi vinapendwa zaidi.
Kuhusu ukarabati wa miundombinu ya barabara kwenye maeneo ya hifadhi Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege hifadhini pamoja na kuweka mazingira wezeshi ili watalii wanapofika wafurahie huduma.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe. Timotheo Mnzava (Mb) ameishauri Serikali kuangalia namna bora ya kurahisisha mchakato wa uwekezaji wa mahoteli kwenye maeneo ya hifadhi ili kuboresha huduma za malazi.