Masaa 24 biashara Kariakoo, hali ya usalama mitaani wanakotoka wateja inaruhusu?

White elephant
mimi Najua watu hawatakuwepo kariakoo saa 8 usiku kufanya manunuzi kwa kuhofia usalama wao wanakotoka na kwenda baada ya manunuzi. Umeme hauko stable jijini, mitaa Haina taa, kamera Wala walinzi. Wavuta bhangi na vishandu wamejaa Kila Kona wakivizia mawindo.
 
Mbona kwenye kumbi za sherehe ni mbali Sana lakini watu tunaenda? Tena na watoto? Mbona kwenye mikesha makanisani tunaenda Tena kwingine nimbali ibada inaisha saa kumi usiku?
Hapo itachochea biashara za mail macasino na sehemu za kupumzika kwa mfano mlimani city ukiamua unakaa zako adi kupambazuke Kuna atakaye kuzuia? Au unakomaa kwenye kituo Cha mwendo Kasi adi jua lichomoze
Nakupa Siri ilala boma soko la mitumba na soko la karume pale watu wa magenge, watu wa mitumba viatu nguo, wanaingia. Kuanzia saa Tisa kufanya shopping ad saa kumi na mbili mtu asha Rudi na mzigo wake mtaani
Maendeleo hayana chama.
Yesu ndio jibu
 
W
H
Hebu ona, wenzako wanaongelea kariakoo wewe unaongelea Mlimani City.

Je, huko kwenye mkesha mnarudi na maboksi ya TV na mafriji mapya? Unadhani kibaka hana akili kama wewe. Kibaka anajua tofauti kati ya anaetoka kwenye mkesha kusali na anaetoka kariakoo shopping.
 
Unalinganisha nyie walevi mbakesha usiku na mkirudi nyumbani mnakuwa mmebeba kitimoto iliyobaki na bia mbili. Sasa kibaka Gani akukamate...


Unalinganisha na kariakoo mtu anaenda Kununua Mzigo wa simu za milion 15 Kwa jumla
 
Mkaamini kabisa 24/7 bussiness?
Maswali ya kujiuliza:-
  1. Wamiliki watakuwa tayari kuongeza wahudumu/wauzaji wa kubadilishana zamu?
  2. Sheria ya kukamata watu usiku na kusema ni wazururaji itaonoshwa?
  3. Mabenki yatafunguliwa usiku?
  4. Kama mchana tu mwanamke akiita kariakoo anashikwa maziwa, matako na kupigiwa miruzi, je usiku ataachwa kuvutwa kichochoroni na kubakwa?
  5. Nani ataweka ulinzi wa magari ya wanunuzi kama mchana tu mateja na vijana wa " Mnadani" wanaiba mirror, wiper na vifuniko vya matairi, usiku je?
 
Unalinganisha nyie walevi mbakesha usiku na mkirudi nyumbani mnakuwa mmebeba kitimoto iliyobaki na bia mbili. Sasa kibaka Gani akukamate...


Unalinganisha na kariakoo mtu anaenda Kununua Mzigo wa simu za milion 15 Kwa jumla
Anafikiri wezi hawana akili
 
Kifupi wamedandia treni kwa mbele, iga vyote tukio na background yake. Think globally and act locally.
 
Mimi natoka Migomigo, kuanzia saa nne au saa tano usiku, nateleza tu mpaka Kariakoo swaafi kabisa, hakuna foleni wala nini.....
 
Kifupi biashara ya masaa 24 inahitaji kiwango kidogo sana cha uhalifu. Kiwango kidogo cha uhalifu kinachangiwa na uwepo wa ajira, ujira mkubwa, elimu ya uraia, ukosefu wa giza mitaani 24/7, kiwango kidogo cha utumiaji wa Madawa ya kulevya, kiwango kidogo cha rushwa, utawala wa sheria na kufungwa kamera mitaani zinazorekodi matukio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…