SoC02 Masaa 3! mtihani wa masaa 3 tu imekuwa sababu ya kuwaacha vijana wengi wa Kitanzania wakitapatapa mtaani bila tumaini

SoC02 Masaa 3! mtihani wa masaa 3 tu imekuwa sababu ya kuwaacha vijana wengi wa Kitanzania wakitapatapa mtaani bila tumaini

Stories of Change - 2022 Competition

Buddah07

New Member
Joined
Aug 27, 2022
Posts
3
Reaction score
2
Ninae andika makala hii ninaitwa Buddah07 kama nilivyojisajiri katika ukurasa huu wa jamii foram. Nina andika makala hii kwa uchungu na maumivu mengi sababu jambo hili ambalo nimechagua kulizungumzia lilinigusa na kuniathiri mimi binafsi pamoja na jopo la vijana wengi Tanzania.

Mtihani wa masaa 3 tu (mtihani wa taifa) kutumika kama kipimo cha uwezo wa wanafunzi Tanzania bila kuzingatia historia yao katika miaka yao yote ya elimu. Na hii ni kwa shule za msingi na sekondari. Je kipimo hiki ni sahihi? Je wanafunzi wanatendewa haki? Acha tuone.

MTAZAMO BINAFSI
Ni kweli kuanzia miaka ya nyuma nchi yetu imekuwa na utaratibu wa kutumia mtihani wa taifa kama kipimo cha uwezo wa na utashi wa wanafunzi mashuleni lakini kwa mtazamo wangu kama mwandishi ninaona hilo si sawa.

Utaratibu huo unawanyima vijana haki ya msingi ya kuendelea na hatua inayofuata kimasomo. Na kipimo hicho kimekuwa kimekuwa chanzo cha vijana wengi kuharibikiwa kisaikolojia . Na kwasababu baada ya mtihani wa mwisho hakuna mtu yeyote anae wakazia uangalifu vijana hao hubaki wagonjwa wa kisaikolojia kwa muda mrefu. Jambo hilo husababisha mdidimio wa vipawa vyao walivyopewa na mungu pamoja na kusizisha ndoto zao.

Inachukua muda kwao kusimama tena pasipo kupata tiba au ushauri wa kitaalamu. Wanaendelea kuugua kwa maumivu makali huku mawazo ya kufeli yakiwaletea kigugumizi katika kila jambo wanalofikiria kulifanya.


MABADIRIKO YANAYOTOKANA NA KUIBUKA KWA CHANGAMOTO KATIKA MIAKA YA ELIMU
Changamoto nyingi zinaweza kuwa sababu ya mabadiliko katika miaka ya elimu. Mfano

1. Mwanafunzi anaweza kuanza shule ya msingi akiwa na uwezo mkubwa katika ufaulu na anaweza kuendelea kufanya vyema pengine kwa miaka 5 mfurulizo yaani mpaka darasa la 5. Baada ya hapo kukatokea changamoto ya kufiwa na wat wake anaowategemea, yaweza kuwa wazazi (baba au mama) au walezi. Matukio hayo yanaweza kupelekea uwezo wa ufaulu wa mwanafunzi kushuka kwasababu ya msongo wa mawazo. Na kama tujuavyo maumivu ya kufiwa hayatoweki haraka katika ubonga hasa kwa watoto. Hilo linaweza kusababisha mwanafunz huyo kufanya vibaya katika miaka yake 2 ya elimu ya msingi yaan darasa 6 na 7 na hilo halimaanishi kwamba mwanafunz huyo hana uwezo katka ufaulu isipo kuwa badiriko limetokea kwasababu ya changamoto zilizo msibu.

Mwanafunzi huyu mwenye uwezo mkubwa lakini aliye athiriwa na vifo vya wazaz wake huachwa mtaani na kuhesabiwa kama mtu asiyestahili kuendelea na hatua inayofuata kielimu. Mtihani wa masaa 3 unamuhukumu na kumuacha mtaani akitapatapa bila tumaini. Fikra yakinifu zinahitajika ili kutafuta ufumbuzi wa suala hili.


2. MFANO UNAONIHUSU MIMI BINAFSI
Mimi binafsi nilihitimu shule ya msingi katika shule ya msingi Ikuti jijini mbeya na nilifanikiwa kufaulu kwa alama za juu.nilifanikiwa kumaliza kama mwanafunzi wa kwanza kishule, mwanafunzi wa 6 kiwilaya na mwanafuzi wa 19 kimkoa. Na hii ilikuwa mwaka 2008.

Baada ya haponilichaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya ufundi Tanga. Nilianza masomo yangu vyema japo changamoto kubwa kwangu ilikuwa lugha ya kiingereza. Kutokana na uwezo mdogo kiuchumi wa wazazi wangu sikufanikiwa kupata mafunzo ya kujiandaa kujiunga na kidato cha kwanza.

Nilipambana sana ili nikae kwenye mstari na kuanza kuelewa masomo ninayo soma kwa lugha ya kigeni. Namshukuru alinisaidia nilianza kuelewa japo si kwa asilimia miamoja lakini nilipambana na nilianza kufanya vizuri. Mtihani wa taifa wa kidato cha pili nilifaulu kwa kupata daraja la kwanza 1/14.

Niliendelea kupambanana hivyo hata nilipokuwa kidato cha tatu. Na kuanzia mwaka huo changamoto zilianza ktika familia yetu. Hali ilizidi kuwa mbaya kiuchumi hivi kwamba nililazimika kubaki shuleni kwa zaidi ya mwaka bila kurudi likizo kwasababu ilikuwa ngumu kwa wazazi wangu kutafuta pesa ya nauli.

Kubwa zaidi maelewano kati ya wazazi wangu yalipotea ndoa yao iliingia matatani. Ugomvi ulikuwa kila siku. Hata niliporudi likizo kati kati ya kidato cha nne mama yangu alikuwa mtu wa kulia kila siku. Baba yangu alikuwa mnyonge sana na alikonda sana. Niligeuka kuwa mshauri kwao ,wote wawili walinieleza kile kinacho wasibu kila mtu akilalamika kwa namna yake. Ilifika hatua nilianza kupewa wosia na kunionyesha nyaraka mbali mbali za msingi kana kwamba wanapoteza maisha karibuni. Hilo liliniathiri sana,likizo yangu ilikuwa mbaya nilikuwa mwenye mawazo sana, saikolojia yangu iliathirika. Kwasababu nilikuwa nimelelewa kidini kama mwanaume nilisimama na kutumia muda huo kuwashauri kila mtu akiwa peke yake na bila kuingilia faragha yao (mambo yandoa)

Licha ya hayo yote nilijitahid sana kusoma, nilitumia nguvu nyingi sana japo saikorojia yangu haikuwa sawa iliathiriwa sana. Nilirud shule kwa ajili ya kufanya mtihan wa mwisho matokeo yalipotoka nilipata ufaulu wa daraja nne 4/28. Nilivunjika moyoyo sana nililia sana kwasababu moyo wangu siku zote unaamini katika kufaulu na si kufeli.

Masaa 3 , mtihani wa masaa 3 tu uliniadhibu na kubaki mtaani nikitapa tapa bila ya kuzingatia historia yangu katika miaka yoote 4 ya masomo.


MAPENDEKEZO YANGU
Kuna sababu nyingi zinazochangia mwanafunzi kufanya vbaya katika mtihani wake wa mwisho.

Ili kupunguza idadi wanaochwa mtaani bila matumaini, vijana wenye uwezo ,vijana wanaotamani kutimiza ndoto zao. Ninapendekeza ufaulu wa mwanafunz upimwe kwa kuzingatia kioindi choote anachokuwa shule. Kwa shule za msing maendeleo ya mwanafunz ya kila mwaka kwa miaka 7 yabebe 60% ya ufaulu wake . Na 40% ya ufaulu ibebwe na mtihani wa mwisho. Vivyo hivyo kwa shule za sekondari ufaulu wa mwanafunz kwa miaka 4 ubebe 60% na mtihani wa mwisho ubebe 40% ya ufaulu.

Hilo litapunguza idadi ya vijana wenye uwezo na vipaji vikubwa kubaki mtaani.

HITIMISHO
Ninapenda kuwashukuru jamii foram kwa kuanzisha jukwaa hili linalowawezesha vijana kueleza hisia zao , Ahsanten sana . Picha za katuni chini zinaonyesha msongo wa mawazo/maumivu ambayo vijana tunayapitia tukiwa mtaani kwa ajili ya kupambania ndoto ambazo zimekatishwa kielimu kwa mtihan wa masaa 3.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom